Tanzania Association taifa ambayo inasimamia swala hili ikisaidiwa na ubalozi, imeyatambua maeneo matatu ambayo Dr Kamara atayatembelea na tarehe na muda kama ifuatavyo:
Inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Luton, Oxford, Milton Keynes, Slough, Bristol, Birmingham, Coventry, Northampton na maeneo mengine ya karibu watahudhuria kongamano la London au Reading.
Vile vile inategemewa kwamba wanajumuiya waishio Leicester, Leeds, Liverpool na maeneo mengine ya kaskazini mwa UK watahudhuria kongamano la Manchester.
Hata hivyo, hakuna kinachomzuia mwananchi kuhudhuria kongamano lolote kati ya hayo hapo juu iwapo tu atatimiza sharti moja kama ilivyoorodheshwa hapo chini.
Angalizo: Ili kuhakikisha kwamba wananchi wengi wanapata nafasi ya kuhudhuria na kushiriki kikamilifu katika hali ya usalama na isiyo na usumbufu, wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika mkoa ambapo kongamano wanalotegemea kuhudhuria litafanyika.
Utaratibu wa kujiandikisha kwa mkoa wa London tumia e-mail ifuatayo: talondon@gmail.com
Kongamano la London litafanyika ubalozini:
Tanzania High Commission
3 Stratford Place W1C 1AS, London.
Kwa maeneo mengine, TA taifa itatoa maelezo zaidi hivi karibuni.
Kwa wananchi Reading, kongamano litafuatiwa na sherehe maalumu - Tanzania Night. Kwa maelezo zaidi tafadhali fuatilia habari hii.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na ziara hii tafadhali wasiliana na TA taifa hapa: watanzaniauk@hotmail.co.uk
07846783365 or 07536497772
KWA NIABA YA UBALOZI NA TA WOTE MNAKARIBISHWA
By Director of Communication - TA National
No comments:
Post a Comment