Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kwa mara nyingine udhamini wake katika mashindano ya Taifa ya mchezo wa Pool mwaka 2010. Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza rasmi tarehe 13 mwezi Julai 2010 katika ngazi za Mikoa.
Bia ya Safari Lager ndio mdhamini mkuu wa mashindano haya.
Akitangaza udhamini wa mashindano ya mwaka huu, Meneja wa bia ya Safari Lager, Fimbo Butallah alisema “Bia ya Safari lager imekuwa mdhamini mkuu wa mchezo wa Pool hapa nchini, na imeweza kuleta mapinduzi ya kweli katika mchezo huu, hivyo ni dhamira ya bia ya Safari kuendelea kudhamini mashindano haya ya Taifa na mengi mengineyo ya mchezo wa pool hapa nchini. Udhamini huu unaanzia ngazi ya mikoa hadi fainali ambazo kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika mjini Arusha mwishoni mwa mwezi Septemba 2010”
Meneja huyo wa Bia ya Safari aliongeza kuwa udhamini wa mwaka huu umeongezeka ukilinganisha na miaka ya nyuma, ikiwa ni pamoja na ongezeko la mikoa shiriki na zawadi za washindi. Akiweka wazi aina za zawadi ambazo washindi wa mwaka huu watapata katika ngazi za mikoa na Taifa Bw. Fimbo alisema.
ZAWADI NGAZI YA MKOA
ZAWADI KWA TIMU
BINGWA ATAPATA SH. 500,000/-
MSHINDI WA PILI ATAPATA SH. 250,000/-
MSHINDI WA TATU ATAPATA SH. 150,000/-
MSHINDI WA NNE ATAPATA SH. 100,000/-
ZAWADI KWA MMOJA MMOJA
KWA UPANDE WA WANAUME BINGWA ATAPATA SH. 250,000/-
MSHINDI WA PILI ATAPATA SH. 150,000/-
MSHINDI WA TATU ATAPATA SH. 100,000/-
MSHINDI WA NNE ATAPATA SH. 50,000/-
KWA UPANDE WA WANAWAKE
BINGWA ATAPATA SH. 150,000/-
MSHINDI WA PILI ATAPATA SH. 100,000
MSHINDI WA TATU ATAPATA SH. 50,000/-
MSHINDI WA NNE ATAPATA SH. 30,000/-
ZAWADI NGAZI YA FAINALI TAIFA
ZAWADI KWA TIMU BINGWA NI SH. 3,500,000/-
MSHINDI WA PILI ATAPATA SH. 2,500,000/-
MSHINDI WA TATU ATAPATA SH. 1,500,000/-
MSHINDI WA NNE ATAPATA SH. 1,000,000/-
ZAWADI WA MMOJA MMOJA KWA UPANDE WA WANAUME
BINGWA ATAPATA SH. 300,000/-
MSHINDI WA PILI ATAPATA SH. 200,000/-
MSHINDI WA TATU ATAPATA SH. 150,000/-
MSHINDI WA NNE ATAPATA SH. 100,000/-
KWA UPANDE WA WANAWAKE
BINGWA ATAPATA SH. 200,000/-
MSHINDI WA PILI ATAPATA SH. 150,000/-
MSHINDI WA TATU ATAPATA SH. 60,000/-
MSHINDI WA NNE ATAPATA SH. 40,000/-
Akiongelea uendeshaji wa mashindano ya mwaka huu, Katibu wa chama cha Pool Taifa Bw. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu kuna ongezeko la Mikoa shiriki kutoka 12 iliyokuwepo mwaka jana hadi 14 na tutaendelea na ushiriki wa mchezaji mmoja mmoja pia (singles) kwa wanaume na wanawake kama ilvyokuwa mwaka uliopita”.
Bw. Amos aliitaja mikoa miwili iliyoongezeka mwaka huu kuwa ni Kagera na Shinyanga. Mikoa mingine inayoshiriki ni Mbeya,Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Mwanza, Iringa, Manyara, Morogoro,Kinondoni, Ilala na Temeke.
Katika ngazi ya mikoa mashindano yataendeshwa kwa club na hatimae Mikoa yote itaunda timu zao za mikoa ambazo zitawakilisha mikoa yao katika fainali za kitaifa zitakazofanyika Mkoani Arusha mwishoni mwa mwezi wa Septemba.
Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Isaac Togocho alisema “Taswira ya mchezo wa pool hapa nchini imebadilika kwa kiasi kikubwa na sasa inwavutia vijana wa kaliba mbalimbali kwani si mchezo wa kupotezea muda tena kama Wengi walivyoudhania, bali ni miongoni mwa michezo inayokua kwa kasi kubwa na kuwapatia kipato wachezaji na vijana kwa ujumla. Ningependa kutoka shukrani za kipekee kwa Safari Lager na TBL kwa ujumla kwa kuweza kuleta mapinduzi haya makubwa katika mchezo wa Pool hapa nchini. Ni dhahiri kuwa mchango wa mdhamini ndio umeleta matunda yote haya ambayo tunayaona hii leo TAPA inaahidi kuendeleza ushirikiano huu mzuri na mdhamini kwa kusimamia na kuendeleza mchezo huu wa Pool hapa nchini.”
Kuhusu TBL
Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.
Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.
Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.
Kuhusu SABMiller
SABMiller plc moja kati ya makampuni makubwa ya bia duniani ikiwa na mikataba ya kutengeneza na kusambaza bia kwenye nchi zaidi ya 60 katika mabara matano. Bia zake ni pamoja na zile za kimataifa kama Miller Genuine Draft, Peroni Nastro Azzurro na Pilsner Urquell vilevile na bia nyingine zinazoongoza kwenye masoko ya ndani ya nchi mbalimbali. Nje ya Marekani, SABMiller ni moja ya kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza vinywaji vya Coca-Cola duniani. Hivi karibuni SABMiller plc ilinunua kampuni ya bia ya Foster’s pamoja na shughuli zake za uzalishaji nchini India.
SABMiller imeorodheshwa kwenye masoko ya hisa ya London na Johannesburg.
Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:
Fimbo Butallah,
Safari Lager Brand Manager,
mailto:fimbo.Buttallah@tzsabmiller.com

No comments:
Post a Comment