Saturday, June 26, 2010

NI MWAKA WA TATA SASA TANGU AMINA ATUTOKE


LEO NI MIAKA 3 KAMILI TOKEA MH. AMINA CHIFUPA WA MPAKANJIA (PICHANI) ATUTOKE. KIFO CHAKE, KILICHOTOKEA GHAFLA, KILITIKISA NCHI NZIMA NA WATANZANIA WOTE KWA JUMLA YAO WALIBAKI MIDOMO WAZI KWA KUONDOKEWA NA MBUNGE HUYU KIJANA ALIYEJIPATIA UMAARUFU KWA MENGI, KUBWA LIKIWA MSIMAMO WAKE WA KUPAMBANA NA JANGA LA MADAWA YA KULEVYA. NA LEO, IKIWA NI SIKU YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA, GLOBU YA JAMII INAJIUNGA NA WANAHARAKATI KAMA AMINA CHIFUPA KUADHIMISHA SIKU HII HUKU TUKIMKUMBUKA MWAHARAKATI HUYU.



ASUBUHI HII KUTAKUWA NA HAFLA YA KUADHIMISHA SIKU YA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA KITAIFA ITAYOANDALIWA NA TUME YA MADAWA KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA ITAYOFANYIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA AMBAPO MGENI RASMI ANATARAJIWA KUWA WAZIRI WA NCHI UTAWALA BORA MH. PHILIP MARMO. HAPANA SHAKA JINA LA AMINA CHIFUPA LITAKUMBUKWA.

No comments:

Post a Comment