Hadi kufikia mei 2010 jumla ya watumishi wa umma 45,846 wamelipwa malimbikiza na mapunjo ya misharara yenye thamani ya shilingi 34,381,059,688.
Hayo yalisemawa leo Bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma Mhe. Hawa Abdulrahman Ghasia wakati akiwasilisha makadirio ya matumizi ya fedha kwa mwaka 2010/2011 mjini Dodoma.
Alifafanua kuwa kati ya idadi hiyo, 20,760 ni Walimu na 25,086 ni watumishi wengine.
‘Kwa upande wa upandishaji wa vyeo, watumishi wa Serikali kuu na Serikali za mitaa wapatao 45,269 walipandishwa vyeo ambayo ni sawa na asilimia 80 ya watumishi 56,586 walioidhinishwa kupandishwa vyeo kwa mwaka 2009/2010’ alisisitiza zaidi.
Alisema vibali vya ajira mpya 44,857 kati aya 45,568 sawa na asilimia 98.4 vya viliyoidhinishwa kwa mwaka 2009/2010 vilivyotolewa kwa waajiri mbali mbali.
Aidha Waziri huyo amesema kuwa katika kuongeza maslahi ya watumishi wa umma katika mwaka wa fedha 2010/2011 Serikali inatarajia kutumia kiasi cha shilingi trilioni 2.332
Fedha hizo zitagaharimia malipo ya mishahara, ajira mpya, upandishaji vyeo na kulipia madini ya malimbikizo ya Serikali kuu na Serikali za mitaa.
Kiasi hicho ni ongezeko kwa shilingi bilioni 558 sawa na asilimia 31.5 ya fedha zilizotengwa kugharimu masilahi na ajira ya umma katika mwaka wa fedha 2009/2010.
‘Serikali inatarajia kuajiri watumishi wapya 49,593 ambapo kipaumbele kitakuwa katika sekta za elimu,afya,kilimo na mifugo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment