Thursday, June 10, 2010

kundi jipya la wanaume wajitambulisha rasmi leo jijini Dar es Salaam

Kampuni ya Mpo Afrika imetangaza kusaini mkataba na kundi jipya litakalokuwa likiitwa Wanaume, likiundwa na wanamuziki walioachwa katika kundi la TMK Wanaume Halisi.

Akizungumza msemaji wa kundi hilo mapema leo ndani ya ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO,Hassan Umande alisema lengo la kuunda kundi hilo jipya ni kwa ajili ya kuendeleza sanaa na kuleta mabadiliko katika anga ya muziki wa kizazi kipya aka bongofleva hapa nchini.

"Mnajua waandishi, kiukweli kuna vikwazo vingi vilitokea mpaka tukaamua kujitenga ,yote hiyo kuepuka migongano ambayo kimsingi si ya lazima kwa sababu saote ni vijana na tunatafuta maisha,kwa hiyo kwa sababu tumetengwa basi tumeamua kuunda kundi la watu sita"'amebainisha Hassani Umande.

Hassani amewataja wasanii watakaounda kundi hilo kuwa ni Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p).

Alisema mpaka sasa wamesharekodi nyimbo tatu ikiwemo, mapenzi kitu gani?, Poa tu pamoja na Mukide.

No comments:

Post a Comment