Thursday, June 17, 2010

Tamasha la Sauti za Busara 2011



Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011


Sauti za Busara ni tamasha la muziki la kimataifa,ambalo hufanyika kila mwezi wa pili Zanzibar,kuonyesha muziki kutoka sehemu zinazo zungumza kiswahili, katika bara la Afrika na pande zote.

Miaka iliyopita ,zaidi ya vikundi 280 vimekwisha shiriki baadhi yao ni Jose Chameleone, Samba Mapangala, Saida Karoli, Natacha Atlas, Didier Awadi, Bassekou Kouyate,Banana Zorro & the B Band, Joh Makini, Nako2Nako Soldiers, Nyota Ndogo,Thandiswa, Culture Musical Club na wengineo wengi.

MWISHO wa kupokea maombi
31 July 2010

Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri , malazi,chakula na matumizi madogo madogo.Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri

Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2011. Wasanii wote watajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa
Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi kutoka kwako kabla ya MWISHO wa kutuma maombi. Maombi yako lazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:

* form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
* nakala moja au mbili ya kazi zako (CD au DVD)
* picha moja au mbili( JPG au karatasi)

Tafadhali tuma nakala,picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo chini.

(Form inaweza kujazwa kupitia mtandao wa intenate)
Call for Artists 2011

No comments:

Post a Comment