Friday, June 4, 2010

JAMANI DUWASA KUNA NAFASI ZA AJIRA

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Dodoma (DUWASA) ni Shirika la Umma lenye dhamana na wajibu wa kutoa huduma ya majisafi na uondoshaji wa majitaka mjini Dodoma. DUWASA ilianzishwa tarehe 01/07/1998 kwa Sheria ya Bunge No. 8 ya mwaka 1997 na kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria Na. 12 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira ya mwaka 2009.

DUWASA inakaribisha maombi ya nafasi za kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa, uzoefu, uzalendo na uchapakazi kwa nafasi zifuatazo:

FUNDI UMEME WA MAGARI (NAFASI MOJA)
Sifa za Elimu
Elimu ya Kidato cha IV/VI pamoja cheti cha elimu ya ufundi wa umeme wa magari na magari kutoka katika Chuo kinachotambulika kisheria. Uzoefu wa mwaka mmoja katika kazi za ufundi wa umeme wa magari.

Majukumu ya Kazi
Kufanya matengenezo ya umeme wa magari, pikipiki na mitambo na kuhakikisha vimewekwa kadi za kumbukumbu za matengenezo.
Kufanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo.
Kufanya ukaguzi wa mifumo ya umeme wa magari, pikipiki na mitambo kila siku na kuhakikisha kuwa inafanya kazi vizuri.
Kutekeleza majukumu mengine ya kiufundi kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake wa Kazi.

KATIBU MUHTASI II (NAFASI MOJA)
Sifa za Elimu
Elimu ya Kidato cha IV/VI pamoja cheti cha elimu ya Uhazili kutoka katika Chuo kinachotambulika kisheria. Uzoefu wa mwaka mmoja katika kazi za Uhazili. Ujuzi wa programu mbalimbali za kompyuta ni wa lazima; ikiwa ni pamoja na uelewa mzuri wa kuandika na kuzungumza lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Majukumu ya Kazi
Kupokea simu, faksi, barua pepe na barua na kutoa taarifa kwa Afisa mhusika.
Kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za ofisi kwa kuzingatia sheria na taratibu.
Kupokea wageni wa ofisi na kuwaelekeza vile inavyopaswa.
Kuandaa rasimu za barua mbalimbali za kiofisi na taarifa mbalimbali kwa usahihi na umakini mkubwa.
Kuchapa kazi mbalimbali za kiofisi kwa njia ya kompyuta.
Kutekeleza majukumu mengine ya kikazi kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake.

MHUDUMU WA MITANDAO YA MAJITAKA II – SEWERAGE ATTENDANTS II (NAFASI NNE)
Sifa za Elimu
Elimu ya Darasa la VII au Kidato cha IV pamoja cheti cha elimu ya ufundi bomba yaani Trade Test Grade III kutoka katika Chuo kinachotambulika kisheria. Uzoefu wa mwaka mmoja katika kazi husika ni wa lazima.

Majukumu ya Kazi
Kuhakikisha kuwa mitandao ya majitaka ambayo imeziba inazibuliwa katika muda mfupi ikiwa ni pamoja na kuondoa taka ngumu kwenye mtandao.
Kufanya utambuzi wa mifuniko ya chemba za mitandao ya majitaka na kuifanyia ukarabati.
Kufanya ukaguzi wa mitandao ya mabomba ya majitaka.
Kuwa na kumbukumbu za kimaandishi za ukaguzi pamoja na matengenezo na kutoa taarifa kwa msimamizi wa kazi.
Kuhakikisha vifaa vya kazi vinatumiwa vizuri, vipo safi na vinahifadhiwa mahali salama.
Kushughulikia malalamiko ya wateja kuhusu huduma ya majitaka na kutoa taarifa kwa Msimamizi wa Kazi.
Kutekeleza majukumu mengine ya kikazi kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake.
FUNDI WA KUTENGENEZA MABOMBA YANAYOVUJA – Leakage Attendants (NAFASI SITA)
Sifa za Elimu
Elimu ya Darasa la VII au Kidato cha IV pamoja cheti cha elimu ya ufundi bomba yaani Trade Test Grade III kutoka katika Chuo kinachotambulika kisheria. Uzoefu wa mwaka mmoja katika kazi husika ni wa lazima.

Majukumu ya Kazi
Kufanya matengenezo ya mitandao ya mabomba ya majisafi ambayo yanavuja.
Kushiriki kwenye kazi mbalimbali za ujenzi wa mitandao ya mabomba ya majisafi.
Kushughulikia malalamiko ya wateja kuhusu upatikanaji wa majisafi na kutoa taarifa kwa Msimamizi wa Kazi.
Kuhakikisha kuwa kazi mbalimbali za kiufundi zinazingatia sheria na taratibu.
Kuwa na kumbukumbu za kimaandishi za ukaguzi pamoja na matengenezo na kutoa taarifa kwa msimamizi wa kazi.
Kuhakikisha vifaa vya kazi vinatumiwa vizuri, vipo safi na vinahifadhiwa mahali salama.
Kutekeleza majukumu mengine ya kikazi kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake.

WAENDESHA PAMPU ZA MAJI -
Pump Attendants II (NAFASI MBILI)
Sifa za Elimu
Elimu ya Darasa la VII au Kidato cha IV pamoja cheti cha elimu ya ufundi bomba yaani Trade Test Grade III kutoka katika Chuo kinachotambulika kisheria. Uzoefu wa mwaka mmoja katika kazi husika ni wa lazima.

Majukumu ya Kazi
Kuwasha na kuzima pampu kwa ratiba iliyopo.
Kurekodi na kutoa taarifa juu ya makatizo ya umeme.
Kurekodi na kutoa taarifa kuhusu kiasi cha majisafi kilichosukumwa kwenda kwa wateja pamoja na hali ya ufanyaji kazi wa mashine (Pressure Gauge Performance).
Kuhakikisha kuwa mazingira ya kituo cha kusukuma maji pamoja na mashine vipo katika hali nzuri na ya usafi wakati wote.
Kuhakikisha vifaa vya kazi vinatumiwa vizuri, vipo safi na vinahifadhiwa mahali salama.
Kutekeleza majukumu mengine ya kikazi kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake.

MAFUNDI MITA - (NAFASI NNE)
Sifa za Elimu
Elimu ya Darasa ya Kidato cha IV pamoja cheti cha elimu ya ufundi bomba yaani Trade Test Grade III kutoka katika Chuo kinachotambulika kisheria. Uzoefu wa miaka miwili katika kazi husika ni wa lazima.

Majukumu ya Kazi
Kufanya matengenezo ya mita goi goi na mita mbovu.
Kutoa taarifa kuhusu wizi wa maji na maji yanayovuja.
Kuhakikisha kuwa mita za maji kwa wateja zina lakili (seal) wakati wote na kutoa taarifa mara moja iwapo mita ya maji imeharibiwa.
Kuhakikisha vifaa vya kazi vinatumiwa vizuri, vipo safi na vinahifadhiwa mahali salama.
Kutekeleza majukumu mengine ya kikazi kama atakavyoagizwa na Msimamizi wake.

7.0 UTARATIBU WA AJIRA
Ajira za Kudumu.

8.0 UMRI KWA NAFASI ZOTE
Miaka 25-40.

9.0 MARUPURUPU
Nafasi zote zina marupurupu mazuri kutegemeana na ujuzi, elimu, uzoefu na uwezo wa kazi.

10.0 NAMNA YA KUOMBA
Barua za maombi zikiwa na wasifu wa waombaji, nakala za vyeti, majina matatu ya watu wanaokufahamu (Credible Referees) pamoja na mawasiliano yako ya posta, simu na barua pepe vitumwe kabla ya tarehe 17 Juni 2010 kwa anwani ifuatayo:

Mkurugenzi Mtendaji
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Dodoma,
S.L.P. 431,
Simu: 026 – 2324245.
Faksi: 026 – 2320060,
DODOMA
E-mail:duwasatz@yahoo.com

ZINGATIA
Wale tu watakaokidhi vigezo na sifa ndio watakaofahamishwa kuhudhuria usaili. Tangazo hili linapatikana pia kwenye Tovuti ya DUWASA ambayo ni: www.duwasa.or.tz

“Wanawake wanahimizwa kuomba nafasi hizi za Ajira”

No comments:

Post a Comment