Saturday, June 26, 2010

STATE HOUSE ZANZIBAR OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

STATE HOUSE ZANZIBAR

OFFICE OF THE PRESS SECRETARY

PRESS RELEASE

Maputo 25.6.2010

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume leo ameshiriki katika Sherehe za kutimiza miaka 35 ya Uhuru wa Msumbiji, zilizofanyika huko mjini Maputo.

Rais Karume aliwasili jana mjini Maputo akiwa amefuatana na mkewe mama Shadya Karume, Waziri wa Utalii, Biasahara na Uwekezaji Mhe. Samia Suluhu Hassan, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Balozi Seif Ali Idd pamoja na maafisa wengine wa serikali.

Rais Karume ambaye amemuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Sherehe hizo za uhuru wa Msumbiji jana jiano alihudhuria chakula cha usiku kilichoandaliwa na Rais wa Msumbiji Mhe. Armando Emilio Guebuza huk Ikulu.

Leo asubuhi Rais Karume alishirikiana na viongozi wengine katika kuweka maua kwenye makaburi ya mashujaa katka uwanja wa mashujaa mjini Maputo.

Miongoni mwa viongozi walioshirki ni mwenyeji wa sherehe hizo Rais Guebuza, na Marais wengine wakiwemo Marais wastaafu kutoka nchi za SADC pamoja na viongozi wengine waalikwa kutoka nchi mbali mbali.

Baada ya hapo Rais Karume alihudhuria sherehe za upokeaji wa mwenge wa umoja katika uwanjawa huru ambapo sherehe kuu za uhuru wa Msumbiji zilifanyika.

Msumbiji imeanzisha mbio za mwenge kwa mara ya mwazo mwaka huu na leo ndio kilele chake baada ya kutembezwa nchi nzima mwenge ambao umepokewa na Rais Guebuza.

Herehe hizo zilifuatana na maombi kutoka dini tofauti, maandamano,ngma za utamaduni, gwaride la vikosi vya ulinzi pamoja na kupigwa mizinga ya kuashiria sherehe hizo.

Katika hotuba yake aliyoitoa Rais Guebuza katika sherehe hizo alieleza mafanikio yaliopatikana nchini humo tokea kupatikana kwa uhuru mwaka 1975.

Alieleza kuwa licha ya changamoo mbali mbali zinazokabiliw na nchi hiyo lakini Msumbiji imeweza kuapta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuimarisha umoja, mshikamano sanjari na amani a utulivu unaoendelea hadi leo hii.

Rais Guebuza aliwapogeza viongozi wote walioshirikiana nae katika sherehe hizo pamoja na kuzipongeza nchi rafiki kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano uliopo kwa muda mrefu ikiwemo Tanzania.

Baada ya sherehe hizo Rais Guebuza aliwalika chakula cha mchana viongozi wote waliohudhuria sherehe hizo akiwemo Rais Karume, Mama Shadya Karume pamoja na ujmbe aliofuatana nao.

Miongo mwa Marais waliohudhuria sherehe hizo ni Rais Mugabe wa Zimbwabwe, Rais Mfalme Mswati wa Swaziland, Rais wa Botswana Generali Seretse Khamaian Khama , Mfalme Letsie wa Lethoto na marais wengine wakiwemo wastaafu Benjamin Mkapa wa Tanzania, Masire wa Botswana, Kaunda wa Zambia, Mbeki wa Afrika Kusini na wengineo.

Maelfu ya wananchi wa Msumbiji walishiriki katika sherehe hizo wakiwemo wanafunzi na wafanyakazi wa taasisi mbali mbali za umma na binafsi. Msumbiji imepata uhuru wake Septemba 25, 1975 kutoka kwa wakoloni wa Kireno.

Rais Karume na ujumbe wake wanatarajiwa kurudi nyumbani kesho.

Rajab Mkasaba

Postal Address: 2422 Tel.:07774274 49. Fax: 024 2231822

E-mail: zanstate@zanzinet.com

No comments:

Post a Comment