Monday, June 21, 2010

Rais Kikwete akichukua fomu Dodoma Leo


Jamani napenda kuwapa updates ya kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma. Mambo ni motomoto sasa hivi, na kwa kweli wana CCM wana kila sababu ya kumdhamini Mh. Jakaya Kikwete.

Zoezi linaloendelea sasa hivi ni kwamba wana CCM wa Mkoa wa Dodoma wanatia saini (kudhamini) kwenye fomu za mgombea wa urais kupitia CCM Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Vijana wa UVCCM ndio wanaoendelea na shughuli hii.
Awali mgombea Urais Mh. Jakaya Kikwete alipita kuwasalimu wana CCM wenzake na kuwashukuru kwa kitendo chao cha kumdhamini ili kuendelea na awamu ya pili ya urais.

Kabla ya hapo, Mgombea pia alipokea michango kutoka vikundi mbalimbali vya wana CCM kumsaidia katika shughuli nzima ya kuzunguka mikoa yote ya Tanzania kuomba udhamini wa kuendelea na uongozi wa CCM ngazi ya juu kabisa.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha fomu kwa wanachama wa CCM muda mfupi baada ya kuichukua mjini Dodoma leo asubuhi.Pemebeni kulia akipiga makofi ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.



Katibu Mkuu wa Chama Cha mapinduzi Yusuf Makamba akimkabidhi foumu ya kugombea Urais, Rais Jakaya Mrisho kikwete katika makao makuu ya CCM mjini dodoma leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment