Wednesday, June 2, 2010

JUNI 5-2010 NI MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA

Tarehe 5, Juni ya kila mwaka Watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuazimisha siku ya mazingira duniani ambapo maadhimisho hayo kuwa ni sehemu ya kumbukumbu mambo mbalimbali ya mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa kuhusu mazingira uliofanyika mwaka 1972 mjini Stockholm Sweden.

Katika mkutano huo pia lilipitishwa azimio la kuunda shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia mazingira duniani (United Nations Enviromental Program) yani (UNEP).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa rais (Mazingira) Dk.Batilda Buriani amesema maendeleo endelevu ya nchi yetu yanategemea sana jinsi tunavyotunza mazingira yetu lakini zaidi ya asilimia 60 ya nchi yetu inakabiliwa na changamoto nyingi ya hali ya jangwa na ukame takribani hekta 220,000 za misitu hufyekwa kila mwaka kwa mahitaji ya nishati hususani mkaa,kilimo kilichoendelevu na biashara ya magogo,uwezo wa malisho katika mikoa mingi umezidiwa na wingi wa mifugo na hivyo kusabisha uharibifu mkubwa wa mazingira na uvamizi wa vyanzo vya maji.

Aidha Dk.Batilda amesema mazingira ya bahari yanaharibiwa kwa kiasi kikubwa hasa kutokana na Uvuvi usioendelevu na uchafuzi wa mazingira ya bahari kwa mfano takwimu zinaonyesha kushuka kwa samaki wanaovuliwa baharini kutoka tani 52,935 mwaka 2001 hadi tani 43,459 mwaka 2007 ambapo takwimu za kimataifa inakadiriwa kuwa miaka 40 ijayo uvuvi wa kibiashara unaweza usiwepo kabisa kutokana na uvuvi usio endelevu(over fishing).

Akihitimisha Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa rais Dk.Batilda Buriani ameziomba taasisi zote,mashirika yasiyo ya kiserikali na wananchi kwa ujumla kutumia fursa ya maadhimisho hayo kwa kushiriki katika shughuli za hifadhi ya mazingira katika maeneo yao na pia akiwataka waganga wa kienyeji ambao ndio watumiaji wakubwa wa misitu katika uchimbaji wa dawa na mabo mengine yanayohusiana na uganga wa kienyeji kulinda misitu.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya misitu kimataifa ni “VIUMBE NI WENGI.DUNIA NI MOJA NA MSTAKABALI MMOJA”Tunza mazingira kwa hifadhi endelevu ya viumbe hai,maadhimisho haya kitaifa mwaka huu kufanyika Mkoani Dodoma katika wilaya ya Bahi.

No comments:

Post a Comment