Afisa habari ya Makamu wa Rais
Mshindi wa tuzo ya Rais ya Hifadhi ya Mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji Nchini bwana Musa Sambe aliyejinyakulia kitita cha shilingi milioni kumi na mbili, katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, ametoa siri ya mafanikio hayo kwa wananchi juu ya suala zima la Utunzaji wa Mazingira.
Bwana Sambe ameeleza siri ya mafanikio yake hayo leo jijini dar es Salaam katika ukumbi wa Habari maelezo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari. Bwana Nyamve ameeleza kuwa amekuwa akifanya juhudi kubwa katika suala zima la utunzaji wa mazingira kwa kuwa na kigezo cha ubunifu, ikiwa ni pamoja na kupanda miti ya matunda, kuchimba kisima cha maji ya kudumu, kutumia nishati mbadala ya jua, majiko banifu na kupanda miche ya miti pamoja na usafi wa mazingira.
“Jitihada zangu hizi zilikuwa hazieleweki kabisa kwa wanakijiji wenzangu lakini kwa kupitia zawadi hii niliyoipata naamini kabisa naweza kuwa mfano katika suala zima la utunzaji wa mazingira, Alifafanua.”
Tuzo hii ya utunzaji wa Mazingira ulihusiha mikoa kumi na sita iliyoandikisha kushiriki ambapo ilishindanishwa katika ngazi mbali mbali ikiwemo ngazi ya kaya. Pamoja na zawadi hiyo ya milioni kumi na mbili, mshindi huyo pia alipata Cheti pamoja na ngao ambapo mshindi wa mkoa ambae ni mkoa wa Iringa ulipata Chei, Kombe na shilingi milioni saba. Mshindi wa ngazi ya Taifa bwana Musa Sambe anatoka katika kijiji cha Mwambengwa wilaya ya Meatu Mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment