Thursday, June 17, 2010

MFUKO WA KUENDELEZA WACHIMBAJI WADOGO





Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja kama kianzio cha Mfuko wa kuendeleza Wachimbaji wadogo nchini.Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mhe. Mazengo Pinda leo Bungeni wakati akiwasilisha mapitio na makadirio ya matumizi ya fedha yake na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2010/2011.
Alisema kuwa pamoja na kuendeleza Mfuko huo pia itaanzisha kitengo maalumu cha kuendeleza wachimbaji hao.Hata hivyo Mhe. Pinda alisema kuwa pamoja na hayo bado kuna tatizo la wachimbaji wadogo kutozingatia taratibu za kisheria na hivyo kuwepo uvamizi wa maeneo, ajali za migodini, uharibifu wa mazingira na migogoro kwenye migodi.
Alitoa wito kwa wachimbaji kufanya shughuli zao kwa kufuata sheria, taaratibu na kanuni za usalama migodini.
Alisema kuwa katika mwaka 2010/2011 serikali itaimarisha Wakala wa Ukaguzi wa Madini kwa kuupatia watumishi mahiri na vitendea kazi vya kisasa.

No comments:

Post a Comment