Saturday, June 19, 2010

ZIFF YAONGEZA AWARD KWA WATANZANIA




Zanzibar International Film Festival (ZIFF) katika kuhakikisha inawapa nafasi wanatasnia ya filamu nchini imeamua kuongeza changamoto zaidi, kama awali ZIFF ilipoamua kufanya Swahili Day kwaajili ya kuonesha filamu za kitanzania tu na sasa imeamua kuoneza changamoto nyingine.

Siku ya Swahili Day itakua ni tarehe 17 Julai, 2010 ambayo pia ni siku ya kutoa tuzo za ZIFF. "Tumeamua kuongeza kitu katika siku hii ili kuweza kuwazuta zaidi watengeneza filamu wa kitanzania, ili wajue jukwaa hili ni lao na pia ZIFF inawajali sana"- Daniel Nyalusi, Meneja wa Tamasha.

ZIFF itatoa tuzo kwa Filamu Bora ya kitanzania na pia Tuzo ya muigizaji bora (Best Tanzania Feature Film and Best Tanzanian Actor/Actress), hii ni katika kuleta changamoto mpya kwa kiwanda cha filamu Tanzania.

Tutatoa ratiba ya filamu zitakazo oneshwa siku hiyo na pia zitaingia moja kwa moja katika kinyang'anyiro cha tuzo hizo. Mpaka sasa filamu zitakazo kuwemo ni Huba, Nani, Usaliti na Happy Caples, Pay Back, Black Sunday, Babra na zingine nyingi ambazo zitagombea tuzo hizo. Filamu hizi ni zile ambazo zimeingia katika kundi la filamu za kitanzania.

Kuna filamu zingine za kitanzania ambazo zimeingia katika kundi la filamu zate katika tuzo za ujumla kwasababu ni fupi ama zimefanywa na watanzania kwa kushirikiana na watu wa nje ndio maana haziwezi kuingia katika kundi hili kama vile Twiga Stars, Ndoto ya Zanzibar, Nipe Jibu, Marafiki, Wanawake 8, Mwamba Ngoma, Stowaways, Tuna Haki na filamu amabyo nimeongoza mimi lakini nimefanya na watu wa Denmark inaitwa Home To Mother.

Tukumbuke Tamasha la Nchi za Jahazi linaanza tarehe 10 na kuisha 18 Julai, 2010.

No comments:

Post a Comment