Monday, June 14, 2010

SHIRIKA LA NYUMBA (NHC) SASA KUFANYA KAZI KIBIASHARA


Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) inatarajia kubadilisha mfumo wake wa kiutendaji na kujiendesha kibiashara zaidi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. John Chiligati leo Bunge mjini Dodoma wakati akifafanua hoja za Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja wakati wa hotuba wa Bajeti kuu ya serikali hivi karibuni.

Alisema kuwa hapo awali NHC ilikuwa inajishughulisha zaidi na ukusanyaji kodi kutoka wapangaji na ukarabati wa majengo ambapo sasa shirika hilo litajikita zaidi katika ujenzi wa nyumba za bei nafuu na kuwauzia wananchi wenye kipato cha chini.

Kwa sasa wakurugenzi wote wakiemo wa mikoani wataajiriwa kwa mkataba katika juhudu ya kuimarisha utendaji wa kazi .

‘‘Bodi mpya ya nyumba iliyoundwa itahakikisha kuwa shirika hili inajenga nyumba nyingi za bei nafuu ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama za nyumba hizo’’ alisema.

Mhe. Waziri alisema baadhi ya nyumba za NHC zitauzwa na zitakazobaki zitatumika kama dhamana ya kutafutia mikopo katika mabenki kwa ajili ya ujenzi wa nyumba zaidi. Alisisitiza kuwa Bajeti ya mwaka huu imelenga zaidi katika kujenga nyumba nyingi kwa ajili ya kuuzwa wananchi.

No comments:

Post a Comment