Tuesday, June 1, 2010

WANANCHI 300 WAVAMIA KITUO CHA POLISI HEDARU NA KUCHOMA MOTO



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Said Mwema akizungumza na waandishi wa habari mchana huu kwenye makao makuu ya jeshi hilo wakati alipozungumzia uvamizi wa kituo cha polisi cha Hedaru uliofanywa na wananchi 300 baada ya kuvamia kituo cha polisi na kuchoma moto pamoja na magari matatu na nyaraka mbalimbali kituoni hapo.

Akifafanua zaidi IGP Said Mwema amesema mnamo tarehe 28-5-2010 mtoto mdogo aitwaye Garce Garce Kelvin mwenye umri wa miaka 5alitoweka nyumbani kwao katika mazingira ya kutatanisha akiwa anatokea shule ya chekechea katika mji mdogo wa Hedaru, baadae katika hatua za ufuatiliaji zilipokelewa taarifa kuwa mtot huyo amepelekwa katika kijiji cha Chome Mlimani katika msitu wa Shengena ambako pia kuna machimbo ya Dhahabu kwa imani za kwamba huenda ameenda kutolewa kafara huko kwa imani za kishirikina.
Tarehe 30-5-2010 mkuu wa kituo akiongozana na wapelelezi walifuatilia taarifa hizo zilizopokelewa kutoka kwa wananchi ambapo katika oparesheni hiyo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wapatao sita na waliendelea kuhojiwa katika kituo cha polisi Same.
Mnamo tarehe 31-5-2010 kulitokea kundi lingine la vijana waliokwenda katika msitu wa Shengena kijiji cha Chome ikidaiwa walipata taarifa kwamba mtoto huyo amepelekwa kutolewa kafara kwenye machimbo ya dhahabu kwa imani za kishirikina, hata hivyo vijana hawa hawakufanikiwa kumpata mtoto badala yake waliwakamata watu nane wanaume saba na mwanamke mmoja waliowakuta na vifaa vya uchimbaji wa madiniya dhahabu na kuwapeleka kituo cha polisi Hedaru.
Majira ya saa mbili usiku tarehe hiyohiyo watuhumiwa wakiw akituoni Hedaru uvumi ulizagaa kwamba watu waliokamatwa na kundi la vijana ndiyo waliohusika na kutoweka kwa Grace Kaelvin hivyo kundi la wananchi 300 walivamia ktuo cha polisi na kuchoma moto kwa nia ya kutaka kuwauwa watuhumiwa hao, hata hivyo hakuna vifo vilivyotokea baada ya polisi kufanikisha kuwatorosha watu hao , leo tarehe 162010 mtoto Grace aliyetoweka aliokotwa sokoni eneo la Pasua na kwasasa anapelekwa kuungana na familia yake zaidi yahapo watuhumiwa watano wamekamatwa kwa kuchoma kituo.
Mwema amesema tabia ya kushambulia vituo vya polisi kwa hisia au kuchukua sheria mkononi kunavuruga amani na utulivu nchini, lakini pia ni uvunjaji wa sheria.

No comments:

Post a Comment