Saturday, May 22, 2010

MAMA KIKWETE CHINA LEO

e
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA,Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya kinyago cha ujamaa Mheshimiwa Wang Zhizheng, 'Vice-chairperson, Chinese People's Political Consultative Committee'aliyemwandalia Mama Salma Kikwete chakula cha mchana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye mjadala wa "Leading Government's Reach to women" pamoja na Mheshimiwa Nguyen Thi Doan,Makamu wa Rais wa Vietnam,katikati, na mwishoni ni Moderator Yang Lan, Afisa Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa 'Sun Media Group'nchini China .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa 20 wa "Global Summit of Women" kwenye ukumbi wa 'Great hall of people'huko Beijing nchini China tarehe 20.5.2010. Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mheshimiwa Maud Olofsson, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Sweden.

Na Mwandishi Maalum,Beijing

MKE wa Rais Mama Salma Kikwete leo atahutubia mkutano wa wanawake wa dunia katika kuelezea mafanikio aliyoyapata katika taasisi yake ya wanawake na maendeleo (WAMA) na juhudi zake binafsi za kusaidia ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Mama Kikwete ambae ametajwa kuwa mfano bora kwa wake wa marais wa Afrika kufuatia taasisi yake ya WAMA kujikita zaidi katika kusaidia jamii na hasa jitihada zake binafsi za kusaidia wanawake,afya, na watoto wanaoishio katika mazingira hatarishi.

Katika mkutano huu wa dunia unafikia kilele chake leo, katika ukumbi wa Marriot city Hall uliopo katikati ya jiji la Beijing na karibu wajumbe 1000 wanaohudhulia mkutano huo wana hamu kubwa ya kusikia mafanikio aliyopata Mama Kikwete katika kutimiza malengo yake ya WAMA.

Juzi katrika ufunguzi wa mkutano huo, Rais wa Global Summit of Woman, Bibi Irene Natividad alimtaja Mama Kikwete kuwa ni mfano bora wa wake wa marais kutoka Afrika na kusema kuwa jitihada zake binafsi zinaweza kuwa fundisha kwa wake wengine wa marais kutoka Afrika na wanwake wengine wanaopenda kusaidia jamii.

Awali jana mchana Mama Kikwete alialikwa katika mkutano wa kuwatambulisha watu mashuhuri waliohudhulia mkutano huo, lakini asilimia kubwa ya maswali yalielekezwa kwa Mama Kikwete baada ya kutakiwa kueleza kwa nini alinzisha taasisi ya WAMA na madhumuni yake makubwa yalikuwa ni nini.

Akijibu maswali kwa kujiamini , Mama Kikwete Kiwete alisema madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa WAMA ni kumuendeleza mwanamke kielimu, kiafya na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wanaishi katika mazingira hatarishi.

Alisema kuwa vitu vingi amekuwa akifanya kupitia taasisi yake ya WAMA kusaidia wanawake wa Kitanzania ikiwemo suala la elimu kwa kuwa ndiyo njia pekee ambayo inaweza kumkwamua mwanamke katika maisha ya chini na hili amekuwa ameanza kwa wasichana wadogo kuwasisitiza umuhimu wa elimu na kujiepusha na mimba za utotoni na hususan swala la kujiepusha na ugongwa wa ukimwi.

Pia alisema katika serikali ya awamnu ya nne inayoongwa na mumewe imeweza kupiga hatua kubwa katika suala la kumtetea mwanamke, kwani wanawake wengi wamekuwa wakipewa nafasi za uongozi kwa asilimia kubwa na hata masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Mama Kikwete aliendelea kusema kuwa mbali ya hiyo serikali imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa benki ya maendeleo ya wanawake ambayo itakuwa hatua muafaka ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

“Ni ushahidi mwingine kwamba serikali yetu inawajali wanawake wa Tanzania na inayodhaamira ya dhati ya kuinua hali zao za kimaisha na kuwepo kwa benkihiyo kumetoa fursa kwa wanawake wa Tanzania kutumia huduma zake za kujiletea maendeleo na kuondokana na umaskini.

Awali mchana jana alikutana na viongozi wa chama cha wafanyabishara wanawake wa China na wale wa Tanzania katika kubadilishana mawazo na kuona uwezekano wa kusiadia katika masuala mbalimbali ya kibiashara katika ya nchi hizi mbili.

No comments:

Post a Comment