Monday, May 24, 2010

KWA SASA MAENDELEO YA MTU BINAFSI KATIKA LUGHA NI KIINGEREZA



Kuna taarifa za kuaminika kwamba ile programu ya matumizi ya kompyuta iliyotengenezwa kwa Kiswahili sanifu cha Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) bado haijapata soko katika matumizi yake kinyume na wengi tulivyotarajia!

Wakati hilo likitokea, ninaamini kabisa wahusika wa program hiyo wao wanaweza kuwa wanaamini na wanamatumaini makubwa kuwa wanainua ufahamu na hata matumizi ya ‘software ‘ hiyo ya Kiswahili.Programu hiyo imeundwa katika mfumo wa programu za Microsoft , sasa basi , ni wazi kwamba kukwama kwa matumizi ya programu hiyo baada ya kuitoa na kuiingiza kwenye soko na kushindwa kutosheleza ni changamoto kubwa.

Binafsi hapa King Kif wa www.kingkif.blogspot.com nawalaumu wapatashaka na isimu na istilahi za Kiswahili na TUKI ambao walishiriki kuunda program hiyo ya Microsoft katika lugha hii.
Eti wao wanaona kwamba tatizo ni la Microsoft yenyewe kwamba wameshindwa kufanya promosheni ya program hiyo!

Eti wao wanaona ama walitarajia kuwa Microsoft yenyewe ichukue jukumu la kuutangaza mpango huo jambo ambalo naliona wanajaribu kukimbia jukumu la lao wenyewe la kuutangaza mapango huo!

Hivi jamani tangu lini jukumu ama kazi ya ya kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ikawa jukumu ama kazi ya Microsoft yenyewe? Yaani wanataka tuamini kwamba sio Kiswahili kama lugha ya watumiaji wa kompyuta ambayo imekataliwa huko sokoni bali eti mtengenezaji wa hiyo programu ndiye kazembea kuitangaza kwenye soko?!

Kwa vyovyote vile King Kif ninaamini kuwa hiyo kampuni ya Microsoft ilichokifanya ni kusikiliza hoja za wadau wa lugha ya Kiswahili ambapo walileta wazo kwamba wanahitaji programu ya Kiswahili katika matumizi ya kompyuta. Microsoft ikakubali na ikaona ni vema , hivyo wakatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu programu hiyo , ndipo wadau wa Kiswahili wakaunda jopo ambalo lilifanya kazi ya ‘kutohoa ‘ yale hasa yalitakiwa kuwa kwenye programu hiyo, nadhani Microsoft waliamini kwamba watumiaji wanahitaji ndio maana wakakubali kuiunda.

Sasa basi , nadhani jamaa zetu hawa wanaona haya tu kutuambia ukweli kuwa mambo yalienda hivyo, na kwa wakati huu wanakaa kimya kwa kuwa nadhani wanafahamu kama wakianza kulijadili na kuweka mambo wazi , litafumua mpango mzima wa kile kinachodaiwa kwamba nguvu nyingi zilitumika kuwa kushawishi Microsoft kukubali kuunda mpango huo!

Hebu kuanzia sasa , wahusika tuambieni ni lini mtaanza kusema ukweli kuhusu kukwama kwa programu hiyo na muache mara moja kuendelea kung’a ng’ania tu nadharia shawishi na fikira dhanifu ama kwa lugha nyingine ‘tafakuri jadidi’. Ninaomba mtoe taarifa rasmi kuhusu mpango wa programu hiyo ya Microsoft ili tuelewe na tuwe na matarajio na kilichofanyika kuliko ukimya huu mnaouendeleza .

Tusipoangalia yatakuwa yale yale kama vile suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya masomo suala ambalo limejadiliwa kwa takriban miongo mitatu lakini hadi wakati huu hakuna cha mno. King kif naanza kushawishika sasa kwamba bado kumbe ni vigumu kwa wasemaji wa lugha ya Kiswahili kupata unafuu kwenye shughuli zetu za uchumi na taaluma kama tutatanguliza lugha yetu ya kuzaliwa.

Ila, japokuwa tunatumia lugha ya Kiingereza kwenye shughuli zetu za taaluma na biashara , lakini bado hatukimudu vema kimombo kama tunavyodhani!!!

Ni kasumba tu kwamba tunasonga kibingwa na hili ni kwa sababu kwa sasa maendeleo ya mtu binafsi katika shughuli zake ni lugha ya Kiingereza.

Bado ninaamini kwamba wadau waliounda programu hiyo ya Microsoft na kutufanya sisi Watanzania tuwe na matumaini makubwa na mprogramu hiyo , sasa wanakwepa nawanatambua fika kwamba bado lugha za kimataifa bado zinatamba dhidi ya lugha yetu ya Kiswahili.


NI MIMI SIGFRED PETER KIMASA KUTOKA WWW.KINGKIF.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment