Wednesday, September 1, 2010

SASA NI USO KWA USO KWENYE FACEBOOK!



Wakati King Kif nakaribia kuhitimu shule ya msingi huko jijini Mwanza mwishoni mwa miaka ya themanini, kaka zangu wajanja kati ya miaka 28 hadi 35 walikuwa na ujanja wa kununua televisheni ili kuiweka ghetto na watu tukajaa kwenye ghetto hizo kucheki mambo.
Acha kabisaaaa!
Ilikuwa ni mzuka sana , kwenye miaka hiyo kulikuwa kuna mastaa walionivutia moja kati hao ni Krs-One ambaye ndiye msanii wa HIP HOP ninaye mheshimu na kupenda kazi zake za sanaa. Pia niliweza kuwafahamu vema mastaa wengine kama Michael Jackson, Madona ,Maradona , Public Enemy , LL Cool J , Cool Moe Dee , NWA na studio ya Def Jam ya Marekani .
Hizo zilikuwa enzi za aina yake kwangu na tuliokuwa watundu tulifanya maujanja kiasi tukafahamika hasa pale jijini Mwanza kwamba sisi ni akina nani!
Hakuna kijana wa miaka hiyo mjanja ambaye alishindwa kuzifahamu taarifa zangu KING KIF ! Sasa basi, kuanzia mwaka 2003 kuna kijana mmoja hapa ulimwenguni anaitwa Mark Zuckerberg .
Huyu jamaa ndiye aliyeunda Facebook , hii ni njia mpya ya mawasilano duniani , mwaka huo alikuwa na umri wa miaka 19 tu.
Wakati huo alikuwa mwanachuo wa Harvard lakini baada ya kufanya ugunduzi huo mara moja akaachana na masomo ili awe bize na utendaji wa Facebook.
Tukio hili linafanana na Bill Gates mbunifu mkuu wa kompyuta kwa mifumo tofauti ya 'windows' ambaye naye alisoma Harvard na aliacha, yaani hakuhitimu.
Face book ni mfumo wa mtandao kwa kutumia kompyuta , ili kila mtu aweze kutumia uwepo wake kwa kuwasiliana ama kukutana uso kwa uso na yeyote yule kwa njia ya mtandao.
Naam, King Kif nipo kwenye masuala haya natumia jina la Sigfred Kimasa .Unaweza kunikaribisha, nitakaribia!

THE FACEBOOK!

The facebook.com unapanuka na kufikia kiwango cha kumeza dunia kwa sasa , ni kama kukutana katika vikundi ,bila urasimu wowote wa kuandaliwa mkutano rasmi na asasi halisi kwa mfano chuo kikuu.

IMETOKA WWW.KINGKIF.BLOGSPOT.COM

No comments:

Post a Comment