TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba ukipokea simu utapata madhara.
Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujum;a kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kuwa hauna ukweli wowote.
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu nyingi duniani, ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu. Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kwa ujumla, kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta, ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote.
Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema.
Uzushi unaoenea upuuzwe kwa kuwa hauna ukweli wowote.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
03 Septemba 2010
No comments:
Post a Comment