RADIO ya Ufaransa leo imezinduliwa rasmi matangazo yake yanayotangazwa kwa Lugha ya Kiswahili kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).
Uzinduzi wa Radio hiyo ulifanyika jijini Dar-es-salaam wakati jopo la viongozi waandamizi wa Idhaa hiyo, waliopokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwatambulisha juu ya matangazo hayo.
Bi. Christine Ockrent, ambaye ni Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Audiovisuel Exterieur de la France,Matangazo ya TV na Radio ya Ufaransa alisema wamechagua lugha kurushia mtangazo hayo kwa sababu inayokuwa ulimwenguni.
“Lugha hiyo, inaendelea kukua na kufikia hatua za juu kujulikana kimataifa baada ya idhaa nyingi kuanza kuitumia,” alisema .
Aliongeza kuwa inasadikiwa kuwa watu kati ya 120 milioni duniani kote hasa waishio chini ya Jangwa la Sahara wanatumia lugha hiyo.
Akitoa maelezo kuhusu uanzishwaji wa radio hiyo , Mwanahabari Mkuu wa Idhaa hiyo Victor Robert Wile alisema kuwa Idhaa hiyo ilianzishwa takribani miezi miwili na nusu, tangu tarehe 5/07/2010 na kulikuwa na mafunzo kwa ajili ya timu inayoendesha matangazo hayo.
Radio hiyo kwa sasa inaendelea kuwa na wasikilizaji wengi nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo matangazo yake yanarushwa kupitia kituo cha TBC taifa chenye masafa ya 94.6FM hivyo kuwezesha kuwafikia watanzania wengi hasa walio vijijini na ofisi yake kuu ya matangazo ipo jijini Dar-es-salaam.
Akitaja utaratibu wa vipindi vya radio hiyo, Mkuu wa Matangazo ya Kiswahili wa radio hiyo, David Coffey alisema, matangazo hayo hurushwa mara tatu kwa siku, asubuhi,mchana na jioni na habari zinazotangazwa na kuhusu bara la Afrika na ulimwenguni kote na habari zake zinahusu uchumi,majarida, michezo na habari za kimataifa.
Hata hivyo alivitaja baadhi ya vipindi vinavyorusha kwa lugha hiyo kuwa ni wimbi la siasa, kinahusu siasa barani aAfrika, siha njema kinachohusu afya bora, gurudumu la uchumi, yaliyojiri, kinachihusu matukio ya wiki nzima na Alhenso France , kinachohusu utamaduni wa Kifaransa.
Pia alizitaja nchi ambazo matangazo ya kituo hicho yanafika kuwa ni pamoja na Tanzania, Kenya,Uganda,Burundi,Rwanda na Kongo.
No comments:
Post a Comment