Tuesday, September 7, 2010

NEC YATUPA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA CCM...

Leo jijini Dar es Salaam Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imetupilia mbali pingamazi lilitolewa na mgombea ubunge wa jimbo la Bahi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Badwel Omar dhidi ya mgombea wa Chama cha Sauti ya Umma(SAU) Bw. Melkezedek Lesaka.

Kwa mujibu wa nakala ya barua iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi jana jijini Dar es salaam kwa Lesaka na Idara ya Habari (MAELEZO) kupata nakala yake imeeleza kuwa matokeo hayo yametokana na Kikao cha NEC cha 31 Agosti mwaka huu.

Ileeleza kuwa vielelezo vilivyoambatanishwa katika rufaa ya mlalamikaji vimeonyesha kuwa Lesaka ametimiza idadi ya wadhamini waliotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Iliongeza kuwa wadhamini walimdhamini kwa hiari yao wenyewe kama ingekuwa kinyume cha hapo walipaswa kupeleka malalamiko yao kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya pingamizi.

Ilisema kuwa kufuatia sababu hizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imerudisha jina la Melkezedek Lesaka kama mgombea halali wa Ubunge wa Jimbo la Bahi kupitia Chama cha SAU.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Bahi, Frank Ernest,alikukubali pingamizi lililotolewa na mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Badwel Omar, kuwa wagombewa wenzake waliwasilisha majina ya wadhamni ambayo yalikuwa yameghushiwa.

Wagombea wawili kati ya watatu wa ubunge katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma wamekata rufaa NEC, kupinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Bahi kuwaengua na kuwaambia kuwa wadhamini wao wameghushi saini na majina.

Wagombea wengine ambao waliokuwa wanaidaiwa kughushi saini za wadhamini ni Eva CUF, Lesaka (Sau) na Miriam Kimboi wa (UPDP), ambaye hakukata rufani.

No comments:

Post a Comment