Monday, September 6, 2010

Uchaguzi Express Kuanza Leo EASTV...



East Africa Television (EATV), itazindua kipindi kipya cha uchaguzi kiitwacho Uchaguzi Express leo tarehe 06/ 09/ 2010 saa tatu kamili usiku.

Kipindi hicho kitakachokuwa kikirushwa hewani moja kwa moja yaani live siku ya Jumatatu na Alhamisi, na kituo hicho namba moja kwa vijana Afrika Mashariki , kwa lengo la kuwaelimisha vijana mambo mbalimbali kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini.

Katika kuhakikisha vijana wanapata muamko na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu, EATV imeandaa mada zaidi ya 15 zitakazojadiliwa kwa kina ili kuwapatia ufahamu wa kutosha vijana.

Mbali na mada kipindi hicho kitakuwa na vipengele mbalimbali ili kufikisha elimu sahihi ya uchaguzi kwa vijana, miongoni mwao ni pamoja na maswali, maigizo, burudani, mashairi na sanaa ya ucheshi.

Pia kipindi cha Uchaguzi Express kitakuwa kikionyesha taarifa mbalimbali za uchaguzi mkuu zilizofanyiwa kazi na timu ya EATV, na kujadiliwa katika kipindi hicho.

Watu mbalimbali wataalikwa kutoa michango yao katika kipindi cha Uchaguzi Express, wakiwemo vijana, wataalam, wanasiasa pamoja na wadau wa vyombo vya habari nchini.

Aidha, watazamaji wa EATV wanaweza kushiriki katika hicho kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kutuma barua pepe ama kutumia blogu.

Mwezi uliopita EATV ilizindua kampeni ya kuhamasisha vijana kupiga kura yenye ujumbe “Kijana Acha Kulalamika, Tumia Kura Yako”, hii ni baada ya kufanya utafiti na kubaini vijana wengi wamekata tamaa na hawana mwamko wa kupiga kura.

No comments:

Post a Comment