Monday, September 20, 2010

BAHATI NASIBU YA KUSISIMUA SUPA PESA YAZINDULIWA RASMI



Bahati nasibu ya kipekee inayojulikana kama SUPA PESA itakayowawezesha watumiaji wa simu kujishindia mamilioni ya pesa kila siku imezinduliwa rasmi nchini jana.

Akiongea kwenye uzinduzi wa bahati nasibu hiyo mkurugenzi wa Supa pesa Bwana Harm Fourie alisema “SUPA PESA ni bahati nasibu inayohusisha ujumbe mfupi wa simu ambayo ni kama mchezo utakaowawezesha wahusika kubahatisha kushinda zawadi za pesa, vocha na nyinginezo nyingi kirahisi tu kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu. Kutakuwa na droo na zawadi za kila siku na ya kila wiki itakayowawezesha wateja kushindania zaidi ya tshs milioni 25 kila wiki.

Supa Pesa inahusisha watumiaji wa simu wa mitandao yote ambayo ni Zain, Tigo, Vodacom na Zantel kwa gharama ya Tshs 500 tu. Baada ya kutuma ujumbe mfupi, mhusika atatumiwa ujumbe wa kumuidhinisha kushiriki kwenye droo. Baada ya hapo mitambo ya kisasa kabisa inachagua washindi bila mpangilio maalumu.

Mr Fourie aliongeza kusema “Supa Pesa itajikita kuisaidia jamiii haswa kwenye maswala ya elimu. Tunaelewa kwamba serikali ina changamoto kubwa sana kwenye hili swala na tunaamini kuwa elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii. Tunapenda kujihusisha moja kwa moja kwenye kutoa mchango utakaoleta mabadiliko katika maisha ya watanzania.

Msemaji mkuu wa Supa Pesa Nancy Sumari alinukuliwa akisema “kutakuwa na droo za kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambapo washindi watatu watajinyakulia Tshs milioni 1 kila siku. Washindi hao watajulishwa ushindi wao kupitia ujumbe mfupi wa simu na watatumiwa hela zao ndani ya masaa 24 kupitia huduma ya malipo ya Mpesa kutoka Vodacom. Pia kutakuwa na droo ya kila Ijumaa itakayohusisha wale wote waliotuma zaidi ya SMS nne (4) katika wiki hiyo,mshindi atajinyakulia Tshs. Milioni Kumi. Mshindi huyu wa wiki atapigiwa simu kupitia redio ya Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wake. Dhumuni kubwa ni kuhakikisha tunawafurahisha wateja wetu kwa kutajirisha maisha ya watu wengi kwa kutoa washindi wengi kila wiki. Bahati nasibu hii ni rahisi sana kushiriki hivyo tunawahimiza watanzania wengi washiriki na kushinda na SUPA PESA!“

Supa pesa imepanga kwenda na wakati na kujumuisha mambo mbalimbali ya kufurahisha kwenye kuendesha mchezo huu ili kuhakikisha kuwa inawaridhisha wateja wake kwa kutajirisha na kubadilisha maisha yao.

No comments:

Post a Comment