Wednesday, September 22, 2010

BIDHAA ZA UTURUKI ZAANDALIWA MAONYESHO


Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umeandaa maonyesho ya pili ya bidhaa za nchi hiyo yatakayoanza Septemba 30 , mwaka huu hadi Oktoba3, mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-salaam.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na balozi wa Uturuki nchini, Tanzania Dk. Sander Gurbuz katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ambapo alisema Tanzania na Uturuki zina uhusiano mzuri hivyo , maonyesho hayo kwani yatasaidia kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo.

Alizitaja baadhi ya bidhaa zitakazoonyeshwa ni za nguo, vyakula ujenzi na zana za kilimo.

Dr. Gurbuz pia alibainisha kuwa Uturuki imewekeza katika sekta mbalimbali nchini kama vile kilimo, afya,madini, elimu , nguo na utalii.

“Tumewekeza nchini Tanzania ili tuweze kuzalidha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi ,” alisema Balozi Gurbuz.

Balozi huyo alisema pia wameandaa mdahalo wa wa wafanyabiashara utakaohusisha nchi za Afrika Mashariki ukaohudhuriwa wajumbe 300 ambao unaotarajiwa kufanyika Ferbuari mwakani mara baada ya uchaguzi mkuu kumalizika. Mdahalo huo unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Alielezea pia katika sekta ya elimu wana utaratibu wa kutoa ufadhili wa masomo ya juu huchukua wanafunzi 35 mpaka 45 kwa mwaka.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakiwaleta madaktari wenye utaalamu mbalimbali kuja kufanya tiba nchini bure wapatao kati ya 25 hadi 35 jijini Dar es Salaam na wana mpango wa wa kuwaleta wengine ambao watatoa tiba hiyo hadi nje ya mkoa huo.

Balozi huyo alisema pia wana mpango wa kuandaa ziara ya waandishi wa habari kutembela nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment