Wednesday, September 1, 2010

DR . HUSSEIN MWINYI: TUNALINDA MIPAKA YA TANZANIA




WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Dk Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia wananchi wa Tanzania kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi (JWTZ) na majeshi mengine kuwa watahakikisha wanalinda mipaka yote ya nchi na kuwa katika hali ya amani na usalama ili wananchi waweze kuingiza na kusafirisha mali zao.

Dk Mwinyi aliyasema hayo wakati wa shehere za miaka 46 ya JWTZ, tokea kuanzishwa kwake kutoka jeshi la mkoloni. Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kijeshi wa nchini na wa nje pamoja na mabalozi, ambapo katika hotuba yake hiyo, Dk Mwinyi alisema Wizara yake itaendelea kusaidia kila linalowezekana ilikuimalisha hali za kiusalama katika mipaka yote ya nchi.

“Wizara yangu kwa kushirikiana na Majeshi yake itaendeleza juhudi za kuhakikisha hali ya usalama wa Wananchi namali zao zinakuwa salama muda wote kwa kuimalisha ulinzi ndani na nje ya mipaka yetu hususani wa baharini na Anga" alisema Dk Mwinyi.

Aliendelea kusema, Majeshi yake kwa kushirikiana na vyanzo mbalimbali vikiwemo vya wananchi wenyewe watahakikisha wanadhibiti vitendo vya kiharamia katika bahari ya Hindi kwa kuzuia waingizaji wa dawa za kulevya, siraha, usafirisha haramu wa binadamu na uingizaji wa meli za kiharamia.

Mambo mengine ni; kuhakikisha wafanyabiashara wanasafirisha mali zao kwa usalama katika mipaka yote ya bahari ambapo ulinzi huo unafanyika kwa kushirikiana na majeshi mbalimbali ya mataifa washiriki.

Katika sherehe hizo, Dk Mwinyi aliweza kujionea vifaa mbalimbali vya jeshi hilo (JWTZ) na namna ya utendaji wake wa kazi , pamoja na kushuhudia zoezi maalum la jeshi hilo katika uokoaji na shughuli za kivita kwa njia ya bahari ambalo liliweza kuvuta watu wengi kwa jinsi walivyo kuwa wakionyesha.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Generali Davis Mwamunyange alimuhakikishia Waziri,Dk Mwinyi kuwa watahakikisha wanafanya kazi kwa hali na uwezo mkubwa kuhakikisha Taifa linakuwa salama muda wote.

“Jeshi lipo imara kwa kila hali hivyo kipindi cha miaka 46 ni fahari kubwa kwa JWTZ hivyo ni kuhakikisha tunafanya kazi kwa hali ya kisasa,umakini na kasi zaidi’ alisema Mwamunyange.

Aidha, katika kujiimalisha na hali ya amani nchi ukiwemo ulinzi wa mipaka ya nchi, alisema kuwa wataweza kuingilia kulinda amani nchini pindi kama itaweza kutokea machafuko, endapo, Jeshi la Polisi nchini limezidiwa na wao wakaombwa na vikundi vya kibinadamu,taasisi ama jeshi hilo la Polisi, ndipo wanaweza kuingilia kati.

“Jeshi la wananchi linaweza kuingia kulinda hali ya amani nchini, pindi kama itatokea machafuko makubwa, lakini kwa kupokea maombi kutoka kwa vikundi vya amani,taasisi za usalama ama jeshi la Polisi lenyewe’ alijibu Jenerali Mwamunyange alipokuwa ameulizwa swali na waandishi.

Maadhimisho hayo ya JWTZ, awali yalikuwa yakifanyika kila baada ya miaka 10,ambapo lilipotimiza miaka 40, waliamua kubadilisha utaratibu huo na kuwa wakiadhimisha kila mwaka kwa Kamandi mbalimbali zilizopo nchini, huku mwaka jana liliazimisha katika Kamandi ya Anga ( Air Wing-Ukonga).

No comments:

Post a Comment