Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” inatarajia kufanya maonyesho maalum katika kusherehekea sikukuu ya EID EL FITRI inayotarajiwa kusherehekewa kati ya siku ya IJUMAA tarehe 10 au siku ya JUMAMOSI tarehe 11 mwaka 2010.
Siku ya IDDI mosi Mchana kuanzia saa nane twanga pepeta inatarajiwa kuanza na onyesho rasmi kwa ajili ya watoto katika ukumbi wa MANGO Garden, ambapo Zawadi nyingi zitatolewa kwa watoto watakaohudhuria, Usiku Twanga pepeta inatarajiwa kuwepo hapo hapo ukumbini Mango Garden onyesho likiwa rasmi kwa watu wazima mara baada ya onyesho la watoto kumalizika.
Siku ya Jumapili tarehe 12 Twanga Pepeta inatarajiwa kumalizia maonyesho yake rasmi kwa ajili ya IDD EL FITRI katika ukumbi wa TCC uliopo Temeke Chang’ombe. Katika onyesho hilo Twanga Pepeta inatarajiwa kutoa Zawadi kwa wapenzi watakaohudhuria ukumbini hapo ambao watasugua visigino vyao vilivyo.
Maandalizi yote kwa ajili ya Maonyesho rasmi ya Kusherehekea sikukuu ya IDD EL FITRI yapo tayari na Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” imejiandaa vilivyo kama kawaida yao kuwapa burudani iliyo katika kiwango cha kimataifa wapenzi wake.
Twanga Pepeta katika maonyesho yote ya Sikukuu ya IDD EL fitri wanatarajiwa kutambulisha nyimbo mpya iliyotungwa na Mwimbaji wao nyota Charles Baba inayoitwa “Dunia Daraja” pia watatambulisha shoo na rapu mpya toka kwa marepa walio katika kiwango cha juu katika Muziki wa Dansi Nchini ambao ni Msafiri Said “DIOUF”, Khalid Chuma “Chokoraa” na Saulo John “Ferguson”.
Twanga Pepeta ambayo imesheheni wanamuziki vijana wenye vipaji vya hali ya juu ambao kwa sasa wameliteka jiji la Dar es salaam vilivyo, mara baada ya kujifua vya kutosha wanakuja na staili mpya ya mwaka huu inayoitwa Twanga.com.. nyimbo mpya…. 2010 inawezekana. Twanga inajidai vilivyo na Vipaji vya Waimbaji Saleh Kupaza, Kalala Jr, Luizer Mbutu a.k.a “Mama B”, Rogart Hegga a.k.a “Caterpillar” Khamis Amigolas, Janeth Isinika na Charles Baba.
Katika maonyesho yote Bendi ya African Stars inatarajiwa kuzidi kutambulisha kibao chake kipya kilichorekodiwa na kusambazwa katika stesheni mbalimbali za Redio kinachojulikana kwa jina Mapenzi hayana kiapo kilichotungwa na Kiongozi msaidizi Saleh Kupaza.
ASET inawapa mkono wa IDD EL FITRI wapenzi, mashabiki na watanzania wotekwa ujumla mara baada ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani salama.

No comments:
Post a Comment