Wednesday, May 19, 2010

Tamasha la Kimataifa la Injili la Desemba 25






KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, iliaandaa tamasha la kimataifa la nyimbo za injili, lililofanyika Desemba 25, mwaka jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Mimi Alex Msama ndiye nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, wa tamasha hilo la aina yake ambapo tamasha hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha waimbaji kutoka nchi za Kenya, Malawi, Uganda, Burundi Zambia na Afrika Kusini.

Lengo la tamasha hilo ilikuwa kuwasaidia watu wenye ulemavu na yatima na wengine wenye mahitaji ambao wanapaswa kusaidiwa katika jamii.

Ujue kuna baadhi ya watu wenye ulemavu ambao wanahitaji misaada mbalimbali, kwa mfano baiskeli, hivyo kampuni yangu ililiona hilo, hivyo tukapanga kuelekeza nguvu kwa walemavu wa mikoani .

Fikiria kuna wengine wanatamani kusoma, lakini kwa kukosa usafiri na huduma nyingine muhimu, wanashindwa, hivyo tumeona ni vizuri kama tutawakumbuka.

Binafsi nimechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa huu wa injili nikiwa kama muasisi wa matamasha ya injili hapa Tanzania , katika tamasha hilo, pia kulikuwa na waimbaji wapya walioingia katika albamu ya Haleluya Collections Volume 5, wakiwamo kutoka Tanzania.

Kamati imeamua kufanya matamasha mara mbili kwa mwaka ikiwa ni kufanyia kazi maoni ya wapenzi na mashabiki wa muziki huo. Kuhusu misaada kwa makundi mbalimbali ya kijamii, kamati yangu imekuwa ikifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kusaidia wenye mahitaji katika jamii.

Alisema, kamati hiyo imekuwa ikimuomba Mungu azidi kuijalia uwezo kwani lengo ni kugawa baiskeli 100 kila mwaka badala ya 70, ilizowahi kugawa na kusomesha yatima. Mbali ya baiskeli, kamati hiyo imewahi kutoa vitanda vya wagonjwa katika hospitali mbalimbali nchini ingawa kwa kipindi hicho hatukuwa tukitangaza hadi pale tuliposhauriwa kufanya hivyo.

Hivyo, kuanzia mwaka jana tumeanza kutangaza hata mapato katika matamasha mbalimbali ili kuwa wazi zaidi, tunadhani kuwa itatujengea imani zaidi kwa jamii.

Aidha, natumia fursa hii kutoa wito kwa watu mbalimbali katika jamii kuguswa na suala hilo, kwani linalenga kusaidia makundi maalumu katika jamii. Sambamba na hilo, natoa wito pia kwa jamii kuunga mkono juhudi za kamati hiyo kwa kununua albamu ya Haleluya Volume 5 iliyoko madukani kwa wakati .

BWANA AWE NANYI.

No comments:

Post a Comment