Thursday, May 27, 2010

BADEA YAIPATIA TANZANIA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 8


Vifijo na vigelegele vilitawala pale Benki ya maendeleo ya uchumi ya Afrika ilivyo badilishana rasmi mkataba wa makubaliano wa kupatiwa Mkopo wa dola za kimarekani milioni 8.

Mkataba huo ulisainiwa leo saa kumi na moja kamili jioni na Kamishna wa Fedha za nje Bw. Ngosha Magonya kwa niaba ya Waziri wa fedha na Uchumi Mhe. Mustafa Haidi Mkulo mjini Abidjan- Ivory cost.

Katika kusaini makubaliano hayo Bw. Abdelaziz Khelef ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Badea alisema kuwa ,mradi una lengo la kuchangia maendeleo ya mtandao wa barabara katika kisiwa cha Zanzibar ili kukidhi mahitaji ya usafiri wa barabara, kusaidia kufufua sekta ya kilimo huko Unguja ambako kuna ardhi nzuri ya kilimo,kusaidia katika mambo ya usafirishaji wa abiria na mazao yao ya kilimo kwa njia ya barabara katika masoko na bandari kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.
Vilevile kusaidia kufufua sekta ya utalii kwa kuimarisha usafiri wa watalii kwenye sehemu za utalii huko Unguja. Na kupigana na umaskini katika maeneo yenye mradi.

mkopo huo uliosainiwa leo hii mjini hapa utalipwa katika kipindi cha miaka 30 ukichanganya na kipindi cha huruma ambacho ni miaka 10 kwa riba ya asilimia 1 kwa mwaka.

Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu-Wizari ya Fedha na Uchumi
Abidjan
26 Mei 2010

No comments:

Post a Comment