Sunday, May 30, 2010

KAMATI ZA SIMBA ZAANZA KAZI

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba imemteua Zakaria Hans-pope kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, alisema kuwa Kamati ya Usajili itakuwa chini ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliyemteua Zakaria Hans-pope huku Katibu wa Kamati hiyo atakuwa ni Mulamu Ngh'ambi, wajumbe ni Swedi Nkwabi, Salim Abdallah, Musleh Al-Rawah, Azim Dewji na Patrick Paul.

Rage alisema Kassim Dewji ameteuliwa kuwa mshauri mkuu wa kamati hiyo ya usajili baada ya kuona mchango wa mra kwa mara katika usajili wa klabu hiyo huku Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' aliyekuwa makamu wa kamati hiyo.

Kaburu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Makamu wake ni Joseph Itang'are, Onesmo Waziri, Said Pamba, Eubert Mhada, Johnson Basasawa na Andrew Tupa.
Kamati ya Mashindano Mwenyekiti ni Hassan Othman 'Hassanoo', Makamu ni Dany Manembe, wajumbe ni Adam Mgoyi, Jerry Yambi, Selemani Zakazaka, Hassan Bantu na Gerald Lukumai.

No comments:

Post a Comment