Friday, May 21, 2010

fainali Zain Africa Challenge 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

May 20, 2010

Kenya yaingiza vyuo vitatu nusu fainali Zain Africa Challenge

Vyuo vitatu kutoka nchini Kenya vimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano yanayoendelea ya Zain Africa Challenge, chemsha bongo ya mtoano ya kimataifa ya Vyuo vikuu kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Africa Nazarene, Chuo kikuu cha Egerton na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta. Chuo Kikuu cha Makerere ndiyo chuo pekee kutoka nje ya Kenya ambaco kimefuzu hatua ya nusu fainali pia.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, Chuo kikuu cha Makerere kutoka Uganda kitakutana na Chuo Kikuu cha Africa Nazarene cha Kenya katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali utakaofanyika jumapili ya wiki hii.

Mchuano mwingine wa nusu fanali utawakutanisha Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta na Chuo Kikuu cha Egerton vyote kutoka Kenya.

Vyuo Vikuu hivyo vinne vilivyofuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali fainali za ZAC ndivyo vinavyowania nafasi ya kuingia fainali ambapo mshindi atapata kitita cha dola za marekani 50,000.

Watazamaji wa Zain Afrika Challenge bado wanafursa ya kushiriki katika mchezo wa Zain kupitia SMS kwa kujibu maswali yanayoulizwa wakati wa mtoano na kujishindia zawadi ya simu mpya za mkononi aina ya Nokia N97 yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane.

Ili kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda namba 15315.

Jumla ya Vyuo Vikuu 100 kutoka nchi nane barani Africa ambazo ni Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia vilichuana katika mtoano wa kitaifa kabla ya kuingia raundi ya kwanza ya fainali ya mtoano wa ZAC nchini Uganda.

Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain zinazolenga kuboresha sekta ya elimu na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhawa kwa wateja wa Zain.

No comments:

Post a Comment