Sunday, October 10, 2010

MSONDO YARUDI DAR ES SALAAM NA KUANZA MAMBO!



BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma , imerejea Dar es Salaam baada ya ziara ya maonyesho matano katika mikoa ya kusini kuanzia Sept 29 mwaka huu ambapo iliweza kukaa huko kwa muda mrefu kwani ni muda mrefu ilikuwa haijaenda kanda hiyo.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Msemaji wa bendi hiyo, Rajabu Mhamila 'Super D' amesema ziara hiyo ilikuwa maalumu kwa ajili ya kuitambulisha albamu yao mpya inayoitwa Huna Shukrani.

"Tukiwa huko tulifanya kazi ya kuwapa burudan wapenzi wetu na walipata nafasi ya kuona mambo mengi yanayohusu bendi yao " . Alisema SUPER D.

Ziara hiyo ilianzia ukumbi wa Bwalo la Maendeleo, Kilwa na Hoteli ya Lindi Oktoba Mosi ambapo Oktoba 2 wakatua Brantare Hall na oktoba 3 wakafanya kweli katika ukumbi wa Madeko Masasi, Oktoba 4 Nachingwea na 5 wafanya mambo yao Nyongoro Hall, Ruangwa.

SUPER D aliendelea kufafanua kwamba mbali na utambulisho wa albamu hiyo bendi hiyo pia ilitoa fursa kwa wapenzi wake wa mikao hiyo kusikia vibao vipya vya Dawa ya Deni kulipa na Lipi Jema vilivyoibwa na wasanii mahiri akiwamo Edo Sanga.

Sasa wamerudi kwa kasi zaidi na hali zaidi ya kuisuka bendi hiyo jana usiku walitumbuiza katika viwanja vya TTC Chan'gombe ambapo kwa kiingilio cha 2000 na leo itafanya kweli ukumbi wa Max Bar, Ilala kwa kiingilio cha 500.



BURUDANI MWANZO MWISHO

P.O Box 15493DAR ES SALAAMPhone no. 0713/0754/0787/0774/ 406938

No comments:

Post a Comment