Friday, October 1, 2010

CHADEMA WAKUTANA NA VIONGOZI WA DINI DAR




Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (katikati) akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum wakati mgombea huyo alipokutana na viongozi mbalimbali wa dini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mgombea mwenza, Said Mzee Said. Picha na habari(Mdau).


A
ASKOFU Tomas Laizer wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati (kulia), akizungumza na mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa, makao makuu ya chama hicho, Kinondoni Dar es Salaam, baada ya ujumbe wa Kamati ya viongozi wa dini nchini akiwemo askofu Laizer, kufanya mazungumzo na viongozi wa CHADEMA jana, ambapo pamoja na mambo mengine walizungumzia mustakabali utakaowezesha uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu, kufanyika kwa amani na kutozusha rabsha baada ya matokeo, kwa kuzingatia mambo kadhaa ikiwemo vyama shiriki kukubali matokeo baada ya uchaguzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na wa tatu ni mgombea ubunge jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama hicho, John Myika.

No comments:

Post a Comment