KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya jamii (NSSF), Ludovic Mrosso ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo, akizungumza na waandishi wa habari, leo mjini Dar es Salaam, kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya mkutano wa siku tatu wa wadau wa shirika hilo, utakaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa mjini Arusha (AICC), kuanzia Februari 2, mwaka huu. Kulia ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) wa NSSF, Said Masimango.
MAANDALIZI ya mkutano wa kwanza wa wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), yamekamilika ambapo hadi kufikia juzi wadau 400 walikuwa wamejisajili kushiriki mkutano huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Ludovic Mrosso ambaye ni Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika hilo alisema, mkutabo huo wa siku tatu utafunbguliwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Februari 2 mwaka huu.
Alisema mkutano huo ambao utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa mjini Arusha (AICC), unatarajiwa kuhudhuriwa na wadai 600 kutoka hapa nchini.
Mrosso alisema, mbali na wadau wa ndani pia NSSF imewaalika wadau kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Burundi, Malaysia na Omani ambao kati yao wamo wataalamu mahiri na wenye uzoefu katika masuala mbalimbali ya Hifadhi za jamii.
Alisema Katika semina hiyo wataalam kutoka Malaysia watatoa mada kuhusu uzoefu wao katika namna ya uenezaji makazi huku wale wa Oman walitoa funzo kuhusu uwekezaji katika masuala ya nishati.
Mrosso alisema, hakuna ada ya ushiriki katika mkutano huo na wadau wanaolengwa ni waajiri, waajiriwa, wakuu wa vitengo vya Utawala na Fedha wa maofisi mbalimbali na Wataalam mbalimbali wa masuala ya hifadhi ya jamii.
Alisema katika mkutano huo aliouita wa kipekee kutakuwa na mada tatu kuu zitakazozungumziwa ambazo ni Uendeshaji na Uwekezaji katika NSSF Hifadhi ya jamii kwa sekta isiyo rasmi na Mamlaka ya usimamizi wa mashirika hifadhi ya jamii."NSSF itahakikisha washiriki wanafaidika na mkutano huo hususan kupitia elimu itakayotolewa na pia watapewa nafasi y a kujadili kwa kina dukuduku zao kuhusu masuala na changamoto mbalimbali zikiwemo shughuli za NSSF kwa jumla," alisema.
No comments:
Post a Comment