Monday, September 27, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kisalimiana na Sister Davita Lumanzi wa Shirika la Wafrancisco wakati alipozungumza na watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania, kwenye Umoja wa Maifa New York ,Septemba 26,2010. Sister Davita Msomi wa fani ya Utawala katika Hospitali na anafanya kazi nchini Marekani.(Picha na Ofisi ya Wziri MKuu)
.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 26, 2010
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tuni Pinda akisalimiana na Meja Ibuge wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokutana na watanzania Waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York Septemba 26, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mzee, Omar Juma Mwilima katika Mkutano wake na Watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Matifa, New York, Septemba 26, 2010. Mzee Mwilima wa Mbezi, Dar es salaam,yuko Malekani kwa mwaliko wa wanae wanoishi huko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

GAZETI LA DIRA YA MTANZANIA JUMATATU LEO





RFI YAZINDUA MATANGAZO YA LUGHA YA KISWAHILI KUPITIA TBC


RADIO ya Ufaransa leo imezinduliwa rasmi matangazo yake yanayotangazwa kwa Lugha ya Kiswahili kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Uzinduzi wa Radio hiyo ulifanyika jijini Dar-es-salaam wakati jopo la viongozi waandamizi wa Idhaa hiyo, waliopokuwa wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuwatambulisha juu ya matangazo hayo.

Bi. Christine Ockrent, ambaye ni Ofisa Mkuu wa Uendeshaji wa Audiovisuel Exterieur de la France,Matangazo ya TV na Radio ya Ufaransa alisema wamechagua lugha kurushia mtangazo hayo kwa sababu inayokuwa ulimwenguni.

“Lugha hiyo, inaendelea kukua na kufikia hatua za juu kujulikana kimataifa baada ya idhaa nyingi kuanza kuitumia,” alisema .

Aliongeza kuwa inasadikiwa kuwa watu kati ya 120 milioni duniani kote hasa waishio chini ya Jangwa la Sahara wanatumia lugha hiyo.

Akitoa maelezo kuhusu uanzishwaji wa radio hiyo , Mwanahabari Mkuu wa Idhaa hiyo Victor Robert Wile alisema kuwa Idhaa hiyo ilianzishwa takribani miezi miwili na nusu, tangu tarehe 5/07/2010 na kulikuwa na mafunzo kwa ajili ya timu inayoendesha matangazo hayo.

Radio hiyo kwa sasa inaendelea kuwa na wasikilizaji wengi nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania ambapo matangazo yake yanarushwa kupitia kituo cha TBC taifa chenye masafa ya 94.6FM hivyo kuwezesha kuwafikia watanzania wengi hasa walio vijijini na ofisi yake kuu ya matangazo ipo jijini Dar-es-salaam.

Akitaja utaratibu wa vipindi vya radio hiyo, Mkuu wa Matangazo ya Kiswahili wa radio hiyo, David Coffey alisema, matangazo hayo hurushwa mara tatu kwa siku, asubuhi,mchana na jioni na habari zinazotangazwa na kuhusu bara la Afrika na ulimwenguni kote na habari zake zinahusu uchumi,majarida, michezo na habari za kimataifa.

Hata hivyo alivitaja baadhi ya vipindi vinavyorusha kwa lugha hiyo kuwa ni wimbi la siasa, kinahusu siasa barani aAfrika, siha njema kinachohusu afya bora, gurudumu la uchumi, yaliyojiri, kinachihusu matukio ya wiki nzima na Alhenso France , kinachohusu utamaduni wa Kifaransa.

Pia alizitaja nchi ambazo matangazo ya kituo hicho yanafika kuwa ni pamoja na Tanzania, Kenya,Uganda,Burundi,Rwanda na Kongo.

Saturday, September 25, 2010

Photo Release




Models shows Mustafa Hasssanali PARFUM D'AMOUR collection durind Maridadi Women Show in Arusha





Models pose with Mustafa Hassanal collection PARFUM D'AMOUR, New Arusha Hotel yesterday.Saphia Ngalapi
Media & PR Manager
Mustafa Hassanali
PO Box 10684, Dar es Salaam, Tanzania
105 Kilimani Road, Kinondoni, Dar es Salaam, Tanzania
(opp. Patricia Metzger Health & Beauty Clinic / near French Embassy)
Tel : +255 (0)22 266 8555
Mobile : +255 (0)712 099 834
Mail : media@mustafahassanali.net
Web : www.mustafahassanali.net
www.swahilifashionweek.com
www.harusitradefair.com
www.twende.info

KIKWETE AFANYA KWELI MUSOMA


Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu yawananchi wa Musoma Mjini kwenye mkutano mkubwa wa kampeni jioni hii.

KWA KUPITIA PROGRAMU YA TUZO POINTI....



Ni kupitia programu ya Tuzo Pointi

Dar es Salaam, Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua programu mpya ya Tuzo Pointi ambayo itawawezesha wateja wake kupata punguzo kubwa la bei wakati wakipata huduma katika sehemu mablimbali kama mahotelini, ofisi za bima na madukani.

Mkuu wa Idara ya Mahusiano ya Wateja, Aika Matiku alisema kwamba huduma hiyo itawawezesha wateja wake kupata punguzo la kati ya asilimia 5 hadi 20 kutoka kwa wauzaji mbalimbali wa bidhaa hapa nchini.

Aliwataja baadhi ya watoaji wa huduma ambao wataanza nao kuwa ni duka la Woolworth, Sunrise Beach Resort na kampuni ya Bima ya Real Insurance. Hoteli za Kunduchi Beach Resort na Zanzibar Beach Resort zitaanza kutoa huduma baada ya kukamilisha taratibu.

Alisema wateja wanaoweza kupata punguzo hilo kubwa ni wale wenye pointi 250 za Tuzo na kuendelea.

“Tumeanzisha huduma hii kwa lengo la kuhakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora na kwa bei nafuu,” alisema.

Alisema huduma hiyo ni sehemu ya programu ya Tuzo Pointi ambayo lengo lake ni kuwazawadia wateja wake waaminifu na kuboresha maisha ya wateja wake.

Alisema mteja anapata pointi kwa njia kuu tatu. Moja ni kwa utumiaji ambapo wateja wa malipo ya kabla watakapotumiaSh 100 na wale wa malipo ya baada watakapotumia Sh 500 wote watapata pointi moja ya Tuzo.

Njia ya pili ni kwa kuongea, akifafanua njia hii alisema mteja akipokea simu kutoka mtandao mwingine atapata pointi moja ya Tuzo

Njia ya tatu ni ile ya mteja wa Vodacom atakapoendelea kuwa mteja wa Vodacom kwa wiki moja huku akitumia simu yake kwa kupokea simu, kupiga, kutuma ujumbe wa maneno au kupokea ujumbe wa maneno atapata pointi nyingine moja ya Tuzo

Alisema kwa wateja wa mikoani wataweza kupata huduma wakiwa huko huko kutoka kwa vituo mbalimbali vya huduma na maduka vilivyoko mikoani.

Thursday, September 23, 2010

MH. MIZENGO PINDA AKUTANA NA RAIS WA LIBERIA NA WAZIRI MKUU WA DENMARK


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Millenia alichokiandaa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmussen (katikati) na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf (kushoto) jijini New York , Septemba 22, 2010.(Picha na Ofisi y a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao cha kujadili maendeleo ya Millenia alichokiandaa kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmussen (kulia ) na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf aliyekaa katikatijijini New York , Septemba 22, 2010.(Picha na Ofisi y a Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf wakifuatilia mkutano wa kujadili maendeleo ya millennia waliouandaa wakishirikiana na Waziri Mkuu wa Denmark L. Lokke Rasmussen jijini New York, Septemba 22, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais wa Liberia, E. Johnson Sirleaf (katikati) wakizungumza na Waziri Mkuu wa Denmark, L. Lokke Rasmusen baada y kikao walichokiandaa cha kujadili maendeleo ya Millenia kilichofanyika jijini New York Septemba 22, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

ILANI YA UCHANGUZI MKUU YA CHADEMA


SOMA KWA KINA ILANI YA CHADEMA.



ILANI

YA UCHAGUZI MKUU WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI, OKTOBA 31, 2010

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

kupitia link ifuatayo:
http://www.chadema.or.tz/uchaguzi/2010/Ilani%202010-2015.pdf

Wednesday, September 22, 2010

KHANGA ZAKALE ....


BIDHAA ZA UTURUKI ZAANDALIWA MAONYESHO


Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania umeandaa maonyesho ya pili ya bidhaa za nchi hiyo yatakayoanza Septemba 30 , mwaka huu hadi Oktoba3, mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-es-salaam.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na balozi wa Uturuki nchini, Tanzania Dk. Sander Gurbuz katika mkutano wake na waandishi wa habari wa ambapo alisema Tanzania na Uturuki zina uhusiano mzuri hivyo , maonyesho hayo kwani yatasaidia kudumisha ushirikiano baina ya nchi hizo.

Alizitaja baadhi ya bidhaa zitakazoonyeshwa ni za nguo, vyakula ujenzi na zana za kilimo.

Dr. Gurbuz pia alibainisha kuwa Uturuki imewekeza katika sekta mbalimbali nchini kama vile kilimo, afya,madini, elimu , nguo na utalii.

“Tumewekeza nchini Tanzania ili tuweze kuzalidha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi ,” alisema Balozi Gurbuz.

Balozi huyo alisema pia wameandaa mdahalo wa wa wafanyabiashara utakaohusisha nchi za Afrika Mashariki ukaohudhuriwa wajumbe 300 ambao unaotarajiwa kufanyika Ferbuari mwakani mara baada ya uchaguzi mkuu kumalizika. Mdahalo huo unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Alielezea pia katika sekta ya elimu wana utaratibu wa kutoa ufadhili wa masomo ya juu huchukua wanafunzi 35 mpaka 45 kwa mwaka.

Aliongeza kuwa wamekuwa wakiwaleta madaktari wenye utaalamu mbalimbali kuja kufanya tiba nchini bure wapatao kati ya 25 hadi 35 jijini Dar es Salaam na wana mpango wa wa kuwaleta wengine ambao watatoa tiba hiyo hadi nje ya mkoa huo.

Balozi huyo alisema pia wana mpango wa kuandaa ziara ya waandishi wa habari kutembela nchi hiyo.

Tuesday, September 21, 2010

RAIS KARUME AKUTANA NA BALOZI WA AFRIKA KUSINI



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume ,akisalimiana na Balozi wa Afrika ya Kusini nchini Tanzania,Dk Thanduyise H.Chiliza,alipofika ikulu mjini Zanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman, Ikulu Zanzibar.

SERIKALI: HAKUTA KUWA NA MGAWO WA UMEME

Kampuni ya Borodino kutoka nchini Urusi ya uwekezaji wa umeme imetia saini na Serikali ya Tanzania mkataba wa mradi wa umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji wenye uwezo wa kuzalisha 222 MV wenye thamani ya dola za Marekani milioni 700.

Makubaliano ya mkataba huo, yalitiwa saini jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya hiyo Razmik Tarverdyan katika ukumbi wa mkukutano wa wizara hiyo jijini Dar es Salaam.

Mradi huo unaojengwa katika eneo la Rumakali ,mkoani Iringa unatarajiwa kukamilika mwaka 2018.

Akizungumzia kuhusu jijitahada za Serikali katika masuala ya umeme, Katibu Mkuu huyo, Jairo alisema wizara yake itahakikisha kuwa Tanzania haitarudi nyuma katika masuala ya nishati hiyo ili iweze kuwa chanzo kikuu cha usambazaji wa umeme kwa Afrika Mashariki na ya Kati.

“Tunataka tuondokane na mgawo wa umeme na kuwa na umeme wa kutosha ambao hutasafirishwa nchi za jirani,” alisisitiza Katibu Mkuu huyo Jairo. Huku akiongeza kuwa hawatarajii kuwa na mgawo wa umeme wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Katibu Mkuu huyo alisema vyanzo vya umeme vitaendelezwa mfano vya maji ili kuifanya Tanzania iwe na umeme wa uhakika, tulivu na safi wenye bei nafuu.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya hiyo Tarverdyan alisema mradi huo ni mkubwa katika uwekezaji wa nishati hiyo katika Afrika Mashariki, hivyo wamewekeza fedha hizo ili kubadilisha maisha ya Watanzania hususan walio kwenye eneo hilo .

Mahitaji halisi ya umeme nchini ni MW 897 wakati uzalishaji wa sasa ni zaidi ya MW 600.

CHUO KIKU CHA ERIC SHIGONGO ...




Mwalimu wa Kimataifa wa somo la Ujasiriamali, Eric James Shigongo amesogeza elimu nyumbani kwako na kukupa mafundisho yenye hadhi ya Chuo Kikuu cha Mtaani.

Shigongo atazindua CD inayoitwa Street University (Chuo Kikuu cha Mtaani) hivi karibuni, lengo likiwa kuwawezesha watu mbalimbali kujifunza somo la Ujasiriamali.

Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Shigongo alisema kuwa ameamua kutoa CD hiyo ili kutoa fursa pana kwa wajasiriamali chipukizi kujifunza mbinu mbalimbali za kunufaika kibiashara.

“Ndani ya CD hiyo natoa elimu bora kabisa. Elimu ya kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wakubwa. Elimu ya kuwakomboa Watanzania katika mambo ya kiuchumi,” alisema Shigongo na kuongeza:

“Nahitaji kuzalisha mabilionea wengi kadiri inavyowezekana, kwahiyo Watanzania wenye kiu ya kutaka kuwa mabilionea, wanaweza kunufaika kupitia CD yangu.”

Monday, September 20, 2010

DIRA YA MTANZANIA JUMATATU WIKI HII




Gazeti lako mahiri la uchambuzi wa mambo ya siasa,michezo burudani na mengineyo linalochapishwa na Kampuni ya Msama Promotions,kesho litakuwa mitaani kwa mara nyingine tena,kama ada yake huwa limesheheni habari kibao za kusisimua.! Usikose jipatie nakala yako mapema kwa shilingi 400/= tu kwa kila kopi.

BAHATI NASIBU YA KUSISIMUA SUPA PESA YAZINDULIWA RASMI



Bahati nasibu ya kipekee inayojulikana kama SUPA PESA itakayowawezesha watumiaji wa simu kujishindia mamilioni ya pesa kila siku imezinduliwa rasmi nchini jana.

Akiongea kwenye uzinduzi wa bahati nasibu hiyo mkurugenzi wa Supa pesa Bwana Harm Fourie alisema “SUPA PESA ni bahati nasibu inayohusisha ujumbe mfupi wa simu ambayo ni kama mchezo utakaowawezesha wahusika kubahatisha kushinda zawadi za pesa, vocha na nyinginezo nyingi kirahisi tu kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu. Kutakuwa na droo na zawadi za kila siku na ya kila wiki itakayowawezesha wateja kushindania zaidi ya tshs milioni 25 kila wiki.

Supa Pesa inahusisha watumiaji wa simu wa mitandao yote ambayo ni Zain, Tigo, Vodacom na Zantel kwa gharama ya Tshs 500 tu. Baada ya kutuma ujumbe mfupi, mhusika atatumiwa ujumbe wa kumuidhinisha kushiriki kwenye droo. Baada ya hapo mitambo ya kisasa kabisa inachagua washindi bila mpangilio maalumu.

Mr Fourie aliongeza kusema “Supa Pesa itajikita kuisaidia jamiii haswa kwenye maswala ya elimu. Tunaelewa kwamba serikali ina changamoto kubwa sana kwenye hili swala na tunaamini kuwa elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya jamii. Tunapenda kujihusisha moja kwa moja kwenye kutoa mchango utakaoleta mabadiliko katika maisha ya watanzania.

Msemaji mkuu wa Supa Pesa Nancy Sumari alinukuliwa akisema “kutakuwa na droo za kila siku kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa ambapo washindi watatu watajinyakulia Tshs milioni 1 kila siku. Washindi hao watajulishwa ushindi wao kupitia ujumbe mfupi wa simu na watatumiwa hela zao ndani ya masaa 24 kupitia huduma ya malipo ya Mpesa kutoka Vodacom. Pia kutakuwa na droo ya kila Ijumaa itakayohusisha wale wote waliotuma zaidi ya SMS nne (4) katika wiki hiyo,mshindi atajinyakulia Tshs. Milioni Kumi. Mshindi huyu wa wiki atapigiwa simu kupitia redio ya Clouds FM kujulishwa kuhusu ushindi wake. Dhumuni kubwa ni kuhakikisha tunawafurahisha wateja wetu kwa kutajirisha maisha ya watu wengi kwa kutoa washindi wengi kila wiki. Bahati nasibu hii ni rahisi sana kushiriki hivyo tunawahimiza watanzania wengi washiriki na kushinda na SUPA PESA!“

Supa pesa imepanga kwenda na wakati na kujumuisha mambo mbalimbali ya kufurahisha kwenye kuendesha mchezo huu ili kuhakikisha kuwa inawaridhisha wateja wake kwa kutajirisha na kubadilisha maisha yao.

TANZANIA IMEPEWA TUZO YA (MDGS) 2010



Tanzania imepewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Millenium Development Goals (MDGs) 2010 : The Global Heabeat kutokana na mafanikio makubwa iliyoyapata katika maendeleo ya Elimu katika sherehe zilizofanyiaka kwenye ukumbi wa Waldorf Astoria Grand Ballroom jijini New York Septemba 19, 2010. Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea tuzo hiyo na kutoka kwa Mmoja wa wasimamizo wa shughuli hiyo na Msanii maarufu , John Schneder. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Tanzania imepewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Millenium Development Goals (MDGs) 2010 The Global Hearbeat kutokana na mafanikio makubwa iliyoyapata katika maendeleo ya Elimu katika sherehe zilizofanyiaka kwenye ukumbi wa Waldorf Astoria Grand Ballroom jijini New York Septemba 19, 2010. Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Balozi wa Tanzania kwenye umoja wa mataifa, Ombeni Sefue wakiwa wameshika tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa: . (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Friday, September 10, 2010

RAIS KARUME ALIHUTUBIA BARAZA LA IDD EL FITRI


Rais wa Baraza na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji DK Amani Abeid Karume,akibadilishana mawazo na makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Pia Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad,(kulia) mara baada ya kulihutubia Baraza la Idd el Fitri katika viwanja vya jumba la Wananchi Forodhani leo.
Picha na Ramadhan Othman,Ikulu Zanzibar.

GAZETI LA DIRA WIKI HII


ALBAMU YA FARAJA NTOBA IPO MADUKANI




Albamu mpya ya muimbaji kutoka kongo anajulikana kwa jina la Faraja Ntaboba, imetoka katika mafumo wa Video na Audio inakwenda kwajina la Mke wa Pili, imetengenezwa na kusambazwa na Msama Promotions. kwa manunuzi ya jumla na rejareja wasiliana na Msama Promotions kwa namba ya simu 0713 616266 begin_of_the_skype_highlighting 0713 616266 end_of_the_skype_highlighting au fika duka la Msama Promotions lililopo mtaa wa mkwepu karibu na roundabout ya Azam- Posta mpya jijini Dar.

Thursday, September 9, 2010

TWENDE- PRESS RELEASE




Saphia Ngalapi
Wed, Sep 8, 2010 at 10:37 PM
To: Joe88tz@yahoo.com
Reply Reply to all Forward Print Delete Show original
FOR IMMEDIATE RELEASE

CONTACT PERSON: Saphia Ngalapi, Media & PR Manager
TELEPHONE NUMBER: +255-712-099834
EMAIL ADDRESS: https://mail.google.com/mail/h/1y0dxtee1iwr4/?v=b&cs=wh&to=media@mustafahassanali.net


To be the most sought out Platform for women entrepreneurs in Tanzania

2 days seminar to Empower, Educate and Enterprise Women

Together we can

More than 100 women entrepreneurs from different part of Tanzania will come together at Diamond Jubilee hall for TWENDE (Tanzania Women Entrepreneurs Networking & Development Expositions). The event will be held on 16 & 17 of September at the Diamond Jubilee Hall in Dar es Salaam,

“TWENDE is a 2 day entrepreneurial exposition which features women who own or run small, medium and large scale businesses including governmental and non governmental organization which shall not only partake in the Exhibition but also participate in a two day Seminar aimed at empowering and enterprising their businesses”. Mustafa explained.

The main objectives for having such platform for women’s entrepreneurs is to promote the role of women in national development by recognizing the potential and achievements of women entrepreneurs, including those with disabilities, in employment creation, it shall Showcase women entrepreneurs as role models, Promoting women’s entrepreneurship development by disseminating information on good business practices, Promoting “Made In Tanzania” product patriotism. TWENDE is an annual Platform in an organized professional format, exhibiting their products and services collectively by creating national, regional and international links between women entrepreneurs.

“Women are born entrepreneurs, they need opportunity and chances to develop their talents, so that is why TWENDE was conceptualized in order to put women efforts together, by making sure that majority of them are able to increase their income generation by using such platforms” Said Mustafa Hassanali founder of TWENDE.

Tanzania Women Entrepreneurs Network & Development Exposition (TWENDE) will bring together women entrepreneurs and activists from Tanzania together under one roof. This shall include a combination of product/service exhibition, and workshop which of latter shall include an interaction program with inspirational role models and women business leaders who have made an outstanding contribution to society and in the business community.


“TWENDE (Tanzania Women Entrepreneurs Network & Development Exposition) is dedicated to providing opportunities for companies to connect, while meeting the business goals of attendees. It is a full networking experience and the very best place to showcase your company's products and services before key decision makers”. Concluded Mustafa.

TWENDE (Tanzania Women Entrepreneurs Network & Development Exposition) is sponsored by 361 Degrees, Delfina, Global Outdoor Media and United States of America Embassy in Dar es Salaam.

MISS TANZANIA......



Picha za warembo (30) wanaotarajiwa kupanda jukwaani Septemba 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City , Dar es salaam katika shindano la kumsaka Vodacom Miss Tanzania 2010.

UCHAGUZI EXPRESS LEO SAA 3 USIKU



Leo Kwenye "UCHAGUZI EXPRESS"
  • Wakati tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi, kutana na wagombea urais wetu. Na je, wananini cha kusema?
  • Na mijadala inaendelea, timu ya Tanganyika ikiwa inaongozwa na Karola Kinasha wakati timu ya Victoria ikiwa inaongozwa na Stara Thomas. Mjadala unahusu Demokrasia na haki za binadamu
  • Kuyaona hayo na mengine mengi usikose kuangalia 'UCHAGUZI EXPRESS' leo saa 3 usiku.

Tuesday, September 7, 2010

NEC YATUPA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA CCM...

Leo jijini Dar es Salaam Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imetupilia mbali pingamazi lilitolewa na mgombea ubunge wa jimbo la Bahi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Badwel Omar dhidi ya mgombea wa Chama cha Sauti ya Umma(SAU) Bw. Melkezedek Lesaka.

Kwa mujibu wa nakala ya barua iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi jana jijini Dar es salaam kwa Lesaka na Idara ya Habari (MAELEZO) kupata nakala yake imeeleza kuwa matokeo hayo yametokana na Kikao cha NEC cha 31 Agosti mwaka huu.

Ileeleza kuwa vielelezo vilivyoambatanishwa katika rufaa ya mlalamikaji vimeonyesha kuwa Lesaka ametimiza idadi ya wadhamini waliotakiwa kwa mujibu wa sheria.

Iliongeza kuwa wadhamini walimdhamini kwa hiari yao wenyewe kama ingekuwa kinyume cha hapo walipaswa kupeleka malalamiko yao kwa Msimamizi wa Uchaguzi kabla ya pingamizi.

Ilisema kuwa kufuatia sababu hizo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imerudisha jina la Melkezedek Lesaka kama mgombea halali wa Ubunge wa Jimbo la Bahi kupitia Chama cha SAU.

Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Bahi, Frank Ernest,alikukubali pingamizi lililotolewa na mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Badwel Omar, kuwa wagombewa wenzake waliwasilisha majina ya wadhamni ambayo yalikuwa yameghushiwa.

Wagombea wawili kati ya watatu wa ubunge katika jimbo la Bahi mkoani Dodoma wamekata rufaa NEC, kupinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Bahi kuwaengua na kuwaambia kuwa wadhamini wao wameghushi saini na majina.

Wagombea wengine ambao waliokuwa wanaidaiwa kughushi saini za wadhamini ni Eva CUF, Lesaka (Sau) na Miriam Kimboi wa (UPDP), ambaye hakukata rufani.

Witnesz Nomination Celebration Party


G5 CLICK COMPANY SHIPPING TANZANIA TO THE WORLD AFFILIATION TO: GLOBAL PUBLISHERS LIMITED Dealing with :-Online Artist Managment :- Website, Blogs, Social Networks - Designing, Development & Maintenance, :-Online Promotion & Advertisement through - Facebook, Myspace, Youtube, Twitter, Google, G5 click :-Graphics - Posters, Flyers, Brochures, Logos, Calenders, etc PHONE: +255-714-204490 begin_of_the_skype_highlighting +255-714-204490 end_of_the_skype_highlighting, +255-713-889878 begin_of_the_skype_highlighting +255-713-889878 end_of_the_skype_highlighting TEL: + 255 222 773 356 begin_of_the_skype_highlighting + 255 222 773 356 end_of_the_skype_highlighting, FAX: + 255 222 773 357 P.O. BOX 7534, DAR ES SALAAM, TANZANIA. WEBSITE: www.G5click.com, EMAIL: info@g5click.com LOCATION: Ali Hassan Mwinyi Shekilango Road, Sinza Bamaga at Global Publishers Offices.

MAGAZETI YA LEO



Monday, September 6, 2010

Uchaguzi Express Kuanza Leo EASTV...



East Africa Television (EATV), itazindua kipindi kipya cha uchaguzi kiitwacho Uchaguzi Express leo tarehe 06/ 09/ 2010 saa tatu kamili usiku.

Kipindi hicho kitakachokuwa kikirushwa hewani moja kwa moja yaani live siku ya Jumatatu na Alhamisi, na kituo hicho namba moja kwa vijana Afrika Mashariki , kwa lengo la kuwaelimisha vijana mambo mbalimbali kuhusiana na uchaguzi mkuu nchini.

Katika kuhakikisha vijana wanapata muamko na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu, EATV imeandaa mada zaidi ya 15 zitakazojadiliwa kwa kina ili kuwapatia ufahamu wa kutosha vijana.

Mbali na mada kipindi hicho kitakuwa na vipengele mbalimbali ili kufikisha elimu sahihi ya uchaguzi kwa vijana, miongoni mwao ni pamoja na maswali, maigizo, burudani, mashairi na sanaa ya ucheshi.

Pia kipindi cha Uchaguzi Express kitakuwa kikionyesha taarifa mbalimbali za uchaguzi mkuu zilizofanyiwa kazi na timu ya EATV, na kujadiliwa katika kipindi hicho.

Watu mbalimbali wataalikwa kutoa michango yao katika kipindi cha Uchaguzi Express, wakiwemo vijana, wataalam, wanasiasa pamoja na wadau wa vyombo vya habari nchini.

Aidha, watazamaji wa EATV wanaweza kushiriki katika hicho kwa kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi wa maandishi, kutuma barua pepe ama kutumia blogu.

Mwezi uliopita EATV ilizindua kampeni ya kuhamasisha vijana kupiga kura yenye ujumbe “Kijana Acha Kulalamika, Tumia Kura Yako”, hii ni baada ya kufanya utafiti na kubaini vijana wengi wamekata tamaa na hawana mwamko wa kupiga kura.

Moto wa Extra Bongo Siku ya Eid El Fitri...




Hi
Hope all is well and everything is kool
We are arranging events for this Eid festive season, the program is as below
on Eid Mosi with Dj PQ . Basically its a new idea that we are introducing,

EID DAY

"Its a Live Dj FuSion and a Live PerforMance from ExTra Bongo Band blazing On StaGe"
Neva Happened Before.... Come and get the really taste a LiVE Fusion
Dj PQ on the TurNtables
ExTra Bongo "Next Level" On the DruMs
Truly an AfriKan FUSION....
Date; EID DAY (Based on sight of the moon)
Time; 4pm till Dawn
Venue: New Msasani Club- (next to Zantel)

Extra
: There will be a Midnight After Party till Dawn with cocktail of House, Techno, DanceHall, RnB, HipHop..etc

EID DAY 2

Extra Bongo Band “Next Level” HoT performance, giving you a launch of the New Singles and introducing NEW members to the Band.
Date; EID DAY-2 (Following the next after Eid Day since its also a public Holiday)
Time; 6pm to Midnight
Venue: TCC Club - Changombe


Regards

Ismail Katumba
C. E. O
I-Noch Company Limited
Cell : +255 787 670 714 begin_of_the_skype_highlighting +255 787 670 714 end_of_the_skype_highlighting
Cell : +255 715 670 714 begin_of_the_skype_highlighting +255 715 670 714 end_of_the_skype_highlighting
Sinza
Shekilango Road
Dar Es Salaam- Tanzania

Sunday, September 5, 2010

EID PARTY RED CARPET AFFAIR READING



SAT 11Th SEPT 2010

EID PARTY RED CAPERT AFFAIR

AT FACE CLUB READING RG1 7JE

DOOR OPEN 10PM-4.30AM

ENTRY £10 ALL NITE

MUSIC BY FINEST DEEJAYS RICHIE, FUGGAFLEX, AND GUEST

ON THE NITE WILL BE OFFERING YOU THE BEST & LATEST AFRO BEATS,RnB,FUNK HOUSE,DANCEHALL +OLD SKUL & MANY MORE......

SO GET YA SWAGGA ON!!! THIS IS A NIGHT TO SHINE WITH THE FRIENDS FROM ALL OVER
GIRLS DRESS TO IMPRESS GUYS COME FULL LOADED

COME AND BE PART OF IT,THIS IS TOTALY A NIGHT NOT TO BE MISSED!!!

HOSTED BY BONGO DEEJAYS AND GERATON PROMOTIONS

for more info visit www.bongodeejays.blogspot.com

MANDHARI YA MWENGE JIJINI DAR LEO

Mabango ya CHAMA CHA MAPINDUZI yamebandikwa kila sehemu ya jiji hili.

Saadane Resigns as Algeria Coach after Tanzania Draw




Rabah Saadane has resigned as Algeria coach, a day after his team's 1-1 home draw with Tanzania in a 2012 Africa Cup of Nations qualifier.

The Algeria Football Federation confirmed that Saadane had tendered his resignation following the disappointing result and that it had been accepted.

Saadane took charge three years ago and steered Algeria to their first World Cup in 24 years in South Africa.

But they went home early after gaining just a point from three group games.

The federation said that Algeria's under-17 coach Abdelhak Ben Chikha will take charge on a caretaker basis.

The 64-year-old previously considered quitting after his team were eliminated from the World Cup at the first hurdle without scoring a goal, but decided to stay on after being awarded a two-year contract extension.

The North Africans finished bottom of Group C after losing to Slovenia and the United States and drawing with England.

However, his extended stay proved short-lived as the Algerians, who reached the semi-finals of the Cup of Nations in Angola in January, opened their 2012 campaign with a dispiriting home draw with the Taifa Stars in Algiers.

The visitors led the Group D favourites when Abdi Kassim fired home a free-kick from 30-yards after 33 minutes.

Adlene Guedioura's equaliser on the stroke of half-time was enough to save some of the Desert Foxes' blushes, but not enough for Saadane to remain as coach.

Saadane has had five stints in all in charge of the national side, including in 1986, when he also led the side to the World Cup finals, in Mexico.


Saturday, September 4, 2010

Jakaya Kikwete Ngerengere leo


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ngerengere, mkoani Morogoro wakimsalimia kwa bashasha mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi kabla ya mgombea huyo kuwahutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni leo asubuhi(picha na Freddy Maro)