Monday, May 31, 2010

NMB kutoa gawio la Shilingi 15 bilioni

WANAHISA wa Benki ya NMB watapata gawio la jumla ya Shilingi 15.7 bilioni kwa mwaka 2009, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.7 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Misheck Ngatunga, amesema mgawo wa kila hisa kwa mwaka utakuwa Shilingi 31.40, ikilinganishwa na Shilingi 30 kwa mwaka 2008.

Alikuwa anawasilisha ripoti ya mwaka 2009 kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa NMB uliofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Ngatunga alisema mwaka 2009 ulikuwa wa changamoto nyingi kutokana na kuongezeza kwa ushindani katika sekta za benki pamoja na mtikisiko wa uchumi duniani, ambao ulikuwa na madhara makubwa katika uchumi wa Tanzania kama kwingineko duniani.

Aliisifu serikali kwa kuandaa mkakati wa kukabiliana na mtikisiko wa uchumi kwa kuendeleza mfuko wa kuokoa na kusaidia sekta na taasisi zilizoathirika na mtikisiko huo.


“Sekta ya fedha ya Tanzania kwa ujumla haikuathirika na mtikisiko huo, na iliendelea kuwa na mtaji wa kutosha na yenye faida. Ingawa athari hizo zilikuwa tofauti kwa kila benki.”Hata hivyo, alisema hali ya uchumi na kushuka kwa viwango vya riba vilichangia kushuka kidogo kwa mapato na faida mwaka 2009, ambapo benki hiyo ilipata faida ya Shilingi 68.04 bilioni (kabla ya kodi), ikilinganishwa na Shilingi 70.94 bilioni mwaka uliotangulia.


Upungufu huo wa faida ni kwa asilimia nne.Wakati huo huo, NMB imedhamiria kuboresha huduma zake na kupunguza msongamo wa wateja katika matawi yake nchini na kuwafikia Watanzania wengi zaidi wanaoshi vijijini.

Katika taarifa yake ya mwaka 2009, benki hiyo yenye mtandao mkubwa nchini imesisitiza kuwa itazingatia zaidi kupunguza muda wa wateja kusubiri katika matawi na ATM, pamoja na kuboresha mikopo.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi alisema pamoja na mafanikio mengi yaliyopatikana katika kipindi kipindi cha mwaka uliopita, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa matawi na mtandao wa ATM kutoka 167 mwaka 2008 hadi 281 mwishoni mwa mwaka 2009, bado wanakabiliwa na changa moto nyingi, ikiwemo tatizo la msongamano wa wateja.

“Nina uhakika kwamba uongozi na wafanyakazi wa NMB watafanikiwa kukabiliana na changamoto hizo,” alisema Ngatunga.Alisema NMB inakusudia kupanua zaidi mtandao wa matawi nchini ili kuweza kujikita zaidi katika msukumo wa ‘Kilimo Kwanza’, mpango wa kuboresha uzalishaji wa kilimo na sekta ya mabadiliko kwa nia ya mapinduzi ya kilimo.

Akizungumza katika mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa NMB, Bern Christiaanse, alisema mtandao wa matawi ya NMB uliongezeka kufikia 133 mwaka 2009, huku matawi mapya nane yakifunguliwa mwaka huo.

Alisema ongezeko hilo ni matokeo ya mkakati wa benki hiyo wa kutoa huduma za kifedha kwa watanzania wengi iwezekanavyo.Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2009, jumla ya raslimali za benki hiyo zilikua kwa asilimia 20.6 kutoka Shilingi 1,384.3 bilioni hadi 1,669.3 bilioni, wakati ambapo mtaji wa benki ulikua kwa asilimia 20.4 kutoka Shilingi 159,689 milioni hadi Shilingi 192,239 milioni.

Taarifa hiyo iliyowasilishwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa NMB ni ya pili tangu benki hiyo iwe kampuni ya umma baada ya kuorodheshwa kwenye soka la hisa la Dar es Salaam.

CNN MULT CHOICE AFRICAN JOUNALIST 2010

Sam Rogers, from South Africa, has been awarded the top prize at this year’s CNN MultiChoice African Journalist 2010 Awards Ceremony.

Sam Rogers, Executive Producer of Factuals – Crime and Investigation Unit, e.tv, won for her story ‘Curse of the Nobody People’, which was chosen from among 2074 entries from 40 nations across the African continent. ‘Curse of the Nobody People’ features on the discrimination and sometimes shocking fate of albinos in Tanzania.

Sam Rogers was one of 27 finalists at the Awards ceremony on Saturday evening and was a winner in the category ‘Television Features Award’.

The Awards, which rotate location each year in tribute to their pan-African credentials, were held at an Awards Ceremony and Gala Evening in Kampala, Uganda this evening, Saturday 29th May 2010.

His Excellency, the President of the Republic of Uganda, General Yoweri Kaguta Museveni; Collins Khumalo, President, MultiChoice Africa and Parisa Khosravi, Senior Vice President of international newsgathering for CNN Worldwide presented Sam Rogers with the Award.

Sam Rogers said: “I’m astounded, very honoured and so glad the story has a platform. People can now see what’s really going on. The truth has been outed.”

Chair of the judging panel, journalist and media consultant Joel Kibazo said: “The journalist told the story with care and sensitivity. She did deep research covering all the angles including the victims, traditional doctors and even the police and the local media. The victims were given a voice and also overcame risks in telling the story. It is a complete piece of work”.


Parisa Khosravi, Senior Vice President of International Newsgathering for CNN Worldwide, said: “Each year, the men and women who enter these awards prove that they have the determination, professionalism and courage to showcase Africa’s stories to the world. In doing so, they highlight the depth and strength of journalism across the continent.”


Collins Khumalo, President MultiChoice Africa, said: “We are very proud to once again partner with CNN International to recognize and encourage excellence in journalism in Africa. The CNN MultiChoice African Journalist of the Year Awards have become one of the continent’s biggest and most coveted journalism awards and celebrate the hard work, talent, sacrifice and the dedication that the best among our journalists commit to their work. The awards have grown significantly over the years and we have witnessed previous winners become internationally recognized for their talent and hard work – watching their rise to fame as respected reporters on Africa has made our investment in these awards truly rewarding. It is a great honour to be in Kampala hosting these awards for the very first time.”


Nico Meyer, Chief Executive Officer, MultiChoice South Africa, said: “As all eyes turn to South Africa this month, it is imperative that journalists are encouraged and supported to tell the African story with passion and excellence. These awards help us to recognise those great stories. This is without a doubt, Africa’s year and we look forward to celebrating more great examples of passion and integrity in journalism next year.”


The evening also recognised Mustafa Haji Abdinur as this year’s recipient of the Free Press Africa Award, for his work in Somalia including the ‘Peace Journalism’ initiative which he launched with the help of fellow Somali journalists. The Award is also in recognition of all the journalists in Somalia who have put their lives at risk in telling the story. There are nine journalists who died during 2009 whilst fulfilling their professional duties.

Sunday, May 30, 2010

Tangazo Uchaguzi wa Viongozi TA London


tangazo uchaguzi wa viongozi TA london
Maandalizi na shughuli za mipango ya kuchagua viongozi wa jumuiya ya watanzania London imekamilika. Uchaguzi utafanyika jumamosi tarehe 05-06-10 kwenye jengo la ubalozi wa Tanzania Uingereza.
Viongozi kumi (10) wa kamati kuu watachaguliwa ili kutuongoza kwa kipindi cha miaka miwili ijayo. Nafasi kumi zitakazokuwa zinawaniwa ni: viongozi watano (5) wakuu (mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu, katibu mwenezi na mweka hazina) pamoja na wajumbe watano ambao kwa pamoja wanaunda kamati kuu.
Taarifa hii na fomu za wagombea zimetumwa kwa wanajumuiya wote wa TA-London kwa njia ya e-mail. Kwa wale ambao hatuna e-mail zao tafadhali tutumie e-mail address yako kwenye address hii: uchaguzi@hotmail.co.uk
Utaratibu wa kugombea ni kama ifuatavyo:
Mtanzania yeyote mwenye sifa za uongozi anaruhusiwa kugombea (soma listi ya sifa za mgombea zilizorodheshwa katika fomu ya mgombea iliyoambatanishwa na taarifa hii kwa wale tulio na email address zao)
Kila anayetarajia kugombea uongozi lazima ajaze fomu ya mgombea (fomu imeambatanishwa na taarifa hii kwa wale tulio na email address zao)
Utaratibu wa kupiga kura ni kama ifuatavyo:
Mtanzania yeyote anayeishi London anaruhusiwa kupiga kuraMpiga kura lazima awe amelipa kiwango cha chini cha ada ya uanachama yaani paundi 5Washindi watapatikana kulingana na wingi wa kura (simple majority)Maelezo zaidi yatatolewa siku hiyo ya uchaguzi.
Sherehe za kuwakabidhi rasmi madaraka viongozi wapya ambazo zilikuwa zifanyike siku hiyo ya uchaguzi zimesogezwa mbele kutokana na ratiba ngumu ya mgeni rasmi na timu yake. Tarehe na utaratibu kamili wa shughuli hii utatangazwa hapo badaye.
Watanzania waishio London tafadhali ni muhimu sana ushiriki katika uchaguzi huu. Viongozi hawa ndio watakaotuongoza kwa kipindi kingine cha miaka miwili.
Tupunguze lawama, tushiriki kwa kugombea na kuwachagua viongozi wenye sifa ili kuiendeleza jumuiya yetu ya London.
Dhumuni: Kuchagua viongozi wa jumuiya ya LondonTarehe: 05-06-10 saa 9 jioni (15pm)Mahali: Tanzania High Commission3 Stratford Place W1C 1AS, London.
Wahusika: Watanzania waishio London.Malipo yote kwa jumuiya ya London kwa sasa tumia account ifuatayo:Bank ni HSB – 79 Piccadilly, London W1J 8EUA/C No: 41 22 96 72Sort Code: 40 05 26.
Tafadhali hakikisha unaandika jina lako pamoja na kuchukua reference number kwa malipo yoyote utakayofanya. Hii ni kwa ajili ya kumbukumbu za jumuiya na kujua malipo yamelipwa na nani.

MKUTANO WA INJILI WA MCHUNGAJI CHRISTOPHER MWAKASEGE WASHINGTON DC

KUTAKUWA NA MKUTANO WA INJILI MJINI WASHINGTON DC UTAKAOHUDUMIWA NA MCHUNGAJI CHRISTOPHER MWAKASEGE NA MAMA DIANA MWAKASEGE
MAHALI:BETHEL CHURCH
8242 GEORGIA AVENUE
SILVERSPRING,
MD 20910

MUDA:SAA 1 USIKU (7PM)


MGENI RASMI
BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI
MHESHIMIWA OMBENI SEFUE


KWA MAELEKEZO PIGA SIMU
240 706 0351
240 338 4917

MAOMBEZI KWA WATU BINAFSI NA TAIFA YATAFANYIKA WOTE MNAKARIBISHWA

KAMATI ZA SIMBA ZAANZA KAZI

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba imemteua Zakaria Hans-pope kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Rage, alisema kuwa Kamati ya Usajili itakuwa chini ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji aliyemteua Zakaria Hans-pope huku Katibu wa Kamati hiyo atakuwa ni Mulamu Ngh'ambi, wajumbe ni Swedi Nkwabi, Salim Abdallah, Musleh Al-Rawah, Azim Dewji na Patrick Paul.

Rage alisema Kassim Dewji ameteuliwa kuwa mshauri mkuu wa kamati hiyo ya usajili baada ya kuona mchango wa mra kwa mara katika usajili wa klabu hiyo huku Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu' aliyekuwa makamu wa kamati hiyo.

Kaburu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Makamu wake ni Joseph Itang'are, Onesmo Waziri, Said Pamba, Eubert Mhada, Johnson Basasawa na Andrew Tupa.
Kamati ya Mashindano Mwenyekiti ni Hassan Othman 'Hassanoo', Makamu ni Dany Manembe, wajumbe ni Adam Mgoyi, Jerry Yambi, Selemani Zakazaka, Hassan Bantu na Gerald Lukumai.

Kaberuka achaguliwa tena kuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)


Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika leo tarehe 27 mwezi mei hapa Abidjan imemchagua tena Bw.Donald Kaberuka kuwa Rais wa Benki hiyo kwa kipindi cha pili. Bw. Kaberuka alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Benki hiyo mwaka 2005.Kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha pili kumetokana na mafanikio makubwa ambayo ameyaleta katika benki hiyo na kuleta maendeleo katika taasisi hiyo muhimu ya kifedha na kwa bara la Afrika. Hii ilibainika kutoka kwa Magavana waliotaka Rais huyo kuendelea na wadhifa wake.Katika kukubali kuthibitishwa kwake katika cheo hicho.
Bw Kaberuka aliwashukuru Magavana hao kwa kuwa na imani na uongozi wake katika benki. “Nina farijika sana kuona kuwa ninyi Magavana mna imani kubwa na mimi hadi kunichagua tena ili niweze kuiongoza taasisi hii muhimu, kwa kweli nina shukuru sana”,alisema." Ningependa kutoa shukrani zangu za pekee kwa uongozi na wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwani wao ndio wamenifikisha hapa kwani mimi ni Rubani tu. Alisema Kaberuka baada ya kuthibitishwa katika nafasi hiyo.“Nilichaguliwa kwa mara ya kwanza miaka mitano iliyopita.
Benki imeongezeka mara mbili .
Lakini katika kipindi cha miaka mitano ijayo, tutajikusanya na kuiweka Afrika katika kiwango cha juu kimataifa",alieleza."Tutajitahidi kuhakikisha kuwa tunafikia mategemeo ya watu wa Afrika. Tutafanya kazi ilitufikie lile lengo la kuwa na bara moja linaloshirikiana kwa kila kitu, tutapambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuhakikisha kuwa tunakuwa na chakula cha kutosha, alisema.Kikosi cha Benki ya Maendeleo ya Afrika kimekuwa na maendeleo makubwa katika shughuli zake za ndani na uongozi, vilevile imelenga zaidi uwajibikaji katika kuleta maendeleo Afrika hasa katika kukuza sekta binafsi, kufadhili miradi inayoshughulikia miundo mbinu, na kusisitiza kuwepo biashara ya pamoja katika kukuza uchumi wa bara la Afrika.Katika ripoti iliyotoka hivi karibuni inayohusu muonekano wa Uchumi katika Bara la Afrika inasema kuwa, ifikapo mwaka 2011 uchumi utakuwa kwa asilimia 5.2 tofauti na kiwango cha sasa cha asilimia 4.5 kwa mwaka 2010.Kwa sababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya Benki ya maendeleo ya Afrika Benki imekuwa na uhaba wa fedha uliosababishwa na mtikisiko wa uchumi. Kwa sababu hiyo basi Magavana pia wametoa uhalalisho wa kuongeza mtaji kwa taasisi zake kwa asilimia 200% hii itasaidia kuendesha miradi na programu ambazo nchi wanachama imezipanga.Chini ya uongozi wa Bw.
Kaberuka Benki imejitahidi kuhakikisha kuwa kunakuwa na mawasiliano ya karibu kati ya nchi zilizoko kwenye ukanda mmoja na sekta binafsi. Aidha benki imefanikiwa kuwa na ofisi katika kila nchi barani Afrika.Magavana waliainisha.
Bw. Kaberuka, ambaye ni Rais wa saba wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, aliapishwa tarehe 1 mwezi septemba mwaka 2005 kwa mara ya kwanza huko Tunisia.Kabla ya kujiunga na Benki, Bw. Kaberuka alikuwa Waziri wa fedha na mipango ya Uchumi wa Rwanda kuanzia mwaka 1997 mpaka 2005, na alitambulika kama Mkuu aliyejenga upya nchi ya Randa ambayo ilikuwa na vita na aliweza kuijenga nchi hiyo kwa kuweka programu nzuri zilizoleta mabadiliko ya uchumi.Alianzisha na kuendeleza maboresho katika uongozi na uchumi mkuu katika mambo ya fedha, mambo ya mabenki, bajeti, miundo muhimu ya nchi ikiwa ni pamoja na benki kuu ya nchi iliyo huru.
Na matokeo ya maboresho hayo ni kukua kwa uchumi wa Rwanda ulio imara na kuiwezesha nchi hiyo kufaidika kwa kufutiwa madeni yake mwezi Aprili mwaka 2005.
Bw. Kaberuka anauzoefu wa zaidi ya miaka 12 katika mambo ya Benki, katika mambo ya fedha na biashara, katika mambo ya biashara ya vitu kimataifa na katika maendeleo ya sekta kabla yakujiunga na serikali.
Akiwa Waziri wa Fedha na mipango kiuchumi, Rais huyu wa Benki ya maendeleo ya Afrika alitumika kama Gavana wa Benki ya Dunia kwa Rwanda, vilevile katika shirika la fedha la kimataifa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.Alisoma Tanzania hadi kidato cha sita na kupata shahada ya kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam.
Vilevile alisoma Uingereza ambapo alipata shahada ya uzamili katika filosofia ya Uchumi na uzamifu katika filosofia ya Uchumi huko chuo kikuu cha Glasgow - Scotland.
Bw. Kaberuka anazungumza vizuri sana Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili.
Ingiahedi MdumaMsemaji Mkuu- Wizara ya fedha na UchumiAbidjan.

Friday, May 28, 2010

TAARIFA KWA UMMA




USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZA MKONONI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa agizo kuwa namba zote za simu za mkononi zisajiliwe Kati ya Julai 1 2009 hadi Desemba 31, 2009; na baadaye muda huo kuongezwa hadi tarehe 30 Juni 2010 ikitamkwa wazi kuwa muda huo wa ujasili hautaongezwa tena.

Sababu za kuanzisha utaratibu wa
kusajili namba za simu zimeelezwa mara kadhaa zikiwemo :

Kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma za mawasiliano
Kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiapo huduma mbalimbali kama M – Pesa, Z-pesa, ZAP na huduma nyingine za malipo ya Ankara kama za Umeme, Maji, Televisheni n.k.
Kuimarisha usalama wa nchi.

Kuyawezesha makampuni ya simu kuwafahamu wateja wao vizuri zaidi ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma kwao.

Wakati tukikaribia tarehe 30 Juni utaratibu umepangwa kupitia makampuni ya simu kuwa kuanzia tarehe 1 Juni 2010 laini yoyote itakayonunuliwa itatumika kwa kupiga au kupokea simu na kutuma au kupokea ujumbe ikiwa imesajiliwa tu na si vinginevyo.

Baada ya saa sita usiku tarehe 30 Juni yaani saa 00.00 kuanzia tarehe 1 Julai, 2010 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa itafungiwa kupiga ,kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi (SMS) kwa siku 90 hadi tarehe 30 Septemba 2010. Katika kipindi hiki cha siku 90 endapo utaisajili namba yako itafunguliwa . Kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo tarehe 30 Septemba zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandao kabisa.

Mnakumbushwa pia kuwa hivi karibuni mswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na posta ulipitishwa na Bunge kuwa sheria. Sheria hiyo inafanya usajili wa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu wa sheria kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai.

Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuyashukuru makampuni ya simu na watumiaji kwa ushirikiano ambao mumeuonesha mpaka sasa kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.
USICHELEWE, SAJILI NAMBA YAKO YA SIMU MAPEMA!
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Thursday, May 27, 2010

NITASOMAJE HII HAPA



NITASOMA SCHOLARSHIP WINNERS MAY 2010
RENILDA AMBROSE CHIMA FULL DURATION SCHOLARSHIP CHIMALA HIGH SCHOOL MBEYA Other winners include;1.SUSAN MILANZINITASOMA LAPTOP 22.

JOYCE MARUWA NITASOMA STATIONERY INSTITUTE OF SOCIAL WORK (HRM) 3RD YEAR3. SAADA S SADALA NITASOMA MOBILET.I.A BBA 1ST YEAR.

BADEA YAIPATIA TANZANIA DOLA ZA KIMAREKANI MILIONI 8


Vifijo na vigelegele vilitawala pale Benki ya maendeleo ya uchumi ya Afrika ilivyo badilishana rasmi mkataba wa makubaliano wa kupatiwa Mkopo wa dola za kimarekani milioni 8.

Mkataba huo ulisainiwa leo saa kumi na moja kamili jioni na Kamishna wa Fedha za nje Bw. Ngosha Magonya kwa niaba ya Waziri wa fedha na Uchumi Mhe. Mustafa Haidi Mkulo mjini Abidjan- Ivory cost.

Katika kusaini makubaliano hayo Bw. Abdelaziz Khelef ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Badea alisema kuwa ,mradi una lengo la kuchangia maendeleo ya mtandao wa barabara katika kisiwa cha Zanzibar ili kukidhi mahitaji ya usafiri wa barabara, kusaidia kufufua sekta ya kilimo huko Unguja ambako kuna ardhi nzuri ya kilimo,kusaidia katika mambo ya usafirishaji wa abiria na mazao yao ya kilimo kwa njia ya barabara katika masoko na bandari kwa ajili ya kuuza nje ya nchi.
Vilevile kusaidia kufufua sekta ya utalii kwa kuimarisha usafiri wa watalii kwenye sehemu za utalii huko Unguja. Na kupigana na umaskini katika maeneo yenye mradi.

mkopo huo uliosainiwa leo hii mjini hapa utalipwa katika kipindi cha miaka 30 ukichanganya na kipindi cha huruma ambacho ni miaka 10 kwa riba ya asilimia 1 kwa mwaka.

Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu-Wizari ya Fedha na Uchumi
Abidjan
26 Mei 2010

Uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Wapiga Kura 2010


TANGAZO MAALUM


KWA WAKAZI WA WA UGHAIBUNI

KUTOKA URBAN PULSE NA BUZZIE PRODUCTION

Mashabiki na Wapenzi wa filamu wa Kitanzania tunapenda kuwataarifu kuwa tumepokea malalamiko yenu kuhusu ubora DVD za filamu ya £ovely Gamble. Kwamba zina giza na sauti si bora na picha zinacheza. Hili tumelichunguza na kugundua ya kuwa linasababishwa na DVD HARAMIA (PIRATE COPIES) zinazouzwa kinyume ya sheria.

Tunaelewa tatizo hili ni sugu dunia nzima na linawanyima thamani ya utamu wa filamu. Vilevile lina changia kudumisha kiwanda cha uzallishaji wa filamu. Kuepukana na adha hii ,Wazalishaji wa £ovely Gamble wanawaomba na kuwashauri kununua filamu hii kutoka kwa DVD za halali zitakazopatikana kuanzia Jumamosi ya tarehe 29-10-2010 kwenye uzinduzi maaluma wa kuchangia yatima wanao ishi na vijirusi wa UKIMWI nyumbani TANZANIA na kwa wakala maalumu watakao tangazwa rasmi siku hiyo

DVD MAALUM “DIRECTORS CUT” WITH BONUS MATERIAL

*FILMMAKERS

*HATAKAMA

*SEXY MAMA

WYCLIFFE VENUE


233 KINGS ROAD READING RG1 4LS. 6.30pm-11.30pm

TCKT IN ADVCE £10 FOR VIP’s SEATS AND £5 FOR STANDARD SEATS. (*VIP TCK HOLDERS GETS FREE AFTER PARTY PASS*)

WOTE MNAKARIBISHWA

Wednesday, May 26, 2010

Matukio ya Rais Karume Ziarani China

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,na Mkewe Mama Shadya Karume,wakipata maelezo walipotembelea Bustai ya Mji Mkongwe wa Shanghai,China YU Garden.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,apata maelezo kutoka afisa wa kampuni ya Huawei,kuhusu utendaji kazi wa kampuni hiyo alipotembela akiwa na ujumbe wake nchini China.

PART YAIVA ARUSHA !

MISS TANZANIA USA Inatafuta Washiriki Sasa!

MISS TANZANIA USA Inatafuta Washiriki Sasa!
MISS TANZANIA USA inatafuta mabinti warembo haraka

Mimi nataka kuandaa Miss Tanzania USA
Natafuta mabinti ambao wanasifa za kuweza kushiriki
hili shindano ambalo litafanyika mwisho wa mwezi july.

VIGEZO

1. UMRI 18-25
2. Awe hajaolewa
3. Anaweza kusafiri nje ya USA na kurudi (awe na makaratasi)
4. Awe anaweza kuongea kingereza vizuru
5. Awe na shape ya kimiss
6. Kama akishinda aweze kukaa Tanzania mwaka mmoja.

Monday, May 24, 2010

DIRA LANGIA SOKONI LEO



May 24, 2010 MCHUMI WA ADB ATOA TAARIFA YA MWELEKEO WA UCHUMI AFRIKA



Mchumi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Mthuli Ncube (katikati)akitoa ufafunuzi kwa waandishi wa habari leo mjini Abidjan juu ya taarifa inaoonyesha mwelekeo wa uchumi barani Afrika. wengine ni Mtafiti na Mchumi wa ADB Peter Walkenhorst ( kushoto) na Mtaalam Msimamizi(lead Expert) wa ADB Nagatte Wade(kulia)
(Picha Ingiahedi mduma Wizara ya Fedha na UchumiTanzania)

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa 45 wa ADB wakimsikiliza jana mjini Abidjan kwa makini Mchumi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Mthuli Ncube ( haypo pichani) wakati akizindua taarifa inaoonyesha mwelekeo wa uchumi barani Afrika.


NI SHOO YA SABAHA MUCHACHO

KWA SASA MAENDELEO YA MTU BINAFSI KATIKA LUGHA NI KIINGEREZA



Kuna taarifa za kuaminika kwamba ile programu ya matumizi ya kompyuta iliyotengenezwa kwa Kiswahili sanifu cha Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) bado haijapata soko katika matumizi yake kinyume na wengi tulivyotarajia!

Wakati hilo likitokea, ninaamini kabisa wahusika wa program hiyo wao wanaweza kuwa wanaamini na wanamatumaini makubwa kuwa wanainua ufahamu na hata matumizi ya ‘software ‘ hiyo ya Kiswahili.Programu hiyo imeundwa katika mfumo wa programu za Microsoft , sasa basi , ni wazi kwamba kukwama kwa matumizi ya programu hiyo baada ya kuitoa na kuiingiza kwenye soko na kushindwa kutosheleza ni changamoto kubwa.

Binafsi hapa King Kif wa www.kingkif.blogspot.com nawalaumu wapatashaka na isimu na istilahi za Kiswahili na TUKI ambao walishiriki kuunda program hiyo ya Microsoft katika lugha hii.
Eti wao wanaona kwamba tatizo ni la Microsoft yenyewe kwamba wameshindwa kufanya promosheni ya program hiyo!

Eti wao wanaona ama walitarajia kuwa Microsoft yenyewe ichukue jukumu la kuutangaza mpango huo jambo ambalo naliona wanajaribu kukimbia jukumu la lao wenyewe la kuutangaza mapango huo!

Hivi jamani tangu lini jukumu ama kazi ya ya kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ikawa jukumu ama kazi ya Microsoft yenyewe? Yaani wanataka tuamini kwamba sio Kiswahili kama lugha ya watumiaji wa kompyuta ambayo imekataliwa huko sokoni bali eti mtengenezaji wa hiyo programu ndiye kazembea kuitangaza kwenye soko?!

Kwa vyovyote vile King Kif ninaamini kuwa hiyo kampuni ya Microsoft ilichokifanya ni kusikiliza hoja za wadau wa lugha ya Kiswahili ambapo walileta wazo kwamba wanahitaji programu ya Kiswahili katika matumizi ya kompyuta. Microsoft ikakubali na ikaona ni vema , hivyo wakatoa ushauri wa kitaalamu kuhusu programu hiyo , ndipo wadau wa Kiswahili wakaunda jopo ambalo lilifanya kazi ya ‘kutohoa ‘ yale hasa yalitakiwa kuwa kwenye programu hiyo, nadhani Microsoft waliamini kwamba watumiaji wanahitaji ndio maana wakakubali kuiunda.

Sasa basi , nadhani jamaa zetu hawa wanaona haya tu kutuambia ukweli kuwa mambo yalienda hivyo, na kwa wakati huu wanakaa kimya kwa kuwa nadhani wanafahamu kama wakianza kulijadili na kuweka mambo wazi , litafumua mpango mzima wa kile kinachodaiwa kwamba nguvu nyingi zilitumika kuwa kushawishi Microsoft kukubali kuunda mpango huo!

Hebu kuanzia sasa , wahusika tuambieni ni lini mtaanza kusema ukweli kuhusu kukwama kwa programu hiyo na muache mara moja kuendelea kung’a ng’ania tu nadharia shawishi na fikira dhanifu ama kwa lugha nyingine ‘tafakuri jadidi’. Ninaomba mtoe taarifa rasmi kuhusu mpango wa programu hiyo ya Microsoft ili tuelewe na tuwe na matarajio na kilichofanyika kuliko ukimya huu mnaouendeleza .

Tusipoangalia yatakuwa yale yale kama vile suala la matumizi ya lugha ya Kiswahili kama lugha ya masomo suala ambalo limejadiliwa kwa takriban miongo mitatu lakini hadi wakati huu hakuna cha mno. King kif naanza kushawishika sasa kwamba bado kumbe ni vigumu kwa wasemaji wa lugha ya Kiswahili kupata unafuu kwenye shughuli zetu za uchumi na taaluma kama tutatanguliza lugha yetu ya kuzaliwa.

Ila, japokuwa tunatumia lugha ya Kiingereza kwenye shughuli zetu za taaluma na biashara , lakini bado hatukimudu vema kimombo kama tunavyodhani!!!

Ni kasumba tu kwamba tunasonga kibingwa na hili ni kwa sababu kwa sasa maendeleo ya mtu binafsi katika shughuli zake ni lugha ya Kiingereza.

Bado ninaamini kwamba wadau waliounda programu hiyo ya Microsoft na kutufanya sisi Watanzania tuwe na matumaini makubwa na mprogramu hiyo , sasa wanakwepa nawanatambua fika kwamba bado lugha za kimataifa bado zinatamba dhidi ya lugha yetu ya Kiswahili.


NI MIMI SIGFRED PETER KIMASA KUTOKA WWW.KINGKIF.BLOGSPOT.COM

The announcement of the 2010 Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership

Time: 11.00 – 12.00 BST (GMT +1), Monday 14 June 2010, registration will be open from 10.00am but please allow a minimum of 30 minutes.
Venue: CBI Conference Centre, First Floor, Centre Point Tower, 103 New Oxford Street London WC1A 1DU

On June 14 2010, this year’s Ibrahim Prize for Achievement in African Leadership will be announced to the world’s media.

The largest individual annual award in the world, the Ibrahim Prize is worth US$5,000,000 over ten years and US$200,000 a year for life. A further US$200,000 a year, for ten years, is also available for public interest activities and good causes espoused by the winner. It is conferred to a democratically elected former Executive Head of State or Government from a sub-Saharan African country who has served their constitutionally mandated term and has left office in the last three years.

The Prize Committee of the Mo Ibrahim Foundation is comprised of:
- Kofi Annan (Chair), former Secretary-General of the United Nations and Nobel Laureate
- Martti Ahtisaari, former President of Finland and Nobel Laureate
- Aïcha Bah Diallo, former Minister of Education in Guinea and Director of Basic Education at UNESCO
- Mohamed ElBaradei, former Director General of the International Atomic Energy Agency and Nobel Laureate
- Graça Machel, Chancellor of the University of Cape Town, and former Minister of Education and Culture in Mozambique
- Mary Robinson, former President of Ireland and former United Nations High Commissioner for Human Rights
- Salim Ahmed Salim, former Secretary-General of the Organisation of African Unity and former Prime Minister of Tanzania

All media are welcome to attend.

For media based outside of London who are unable to attend:
- A press release will be distributed at the exact time of the announcement, approximately 1015 GMT
- Photos from the announcement will be made available on the Foundation’s website immediately after the press conference, by 1230 GMT.
- Audio clips from the announcement will be available on the Foundation’s website immediately after the press conference, by 1230 GMT. These will also be distributed to radio stations in Africa.
- A Video News Release will be available via Reuters distribution service or can be couriered to TV stations on request (please contact chande.r@moibrahimfoundation.org)
Media outlets interested in these resources should send an email to chande.r@moibrahimfoundation.org indicating what they would like to receive.

To register, request interviews, organise camera positions, or ask any questions, please contact:
Hannah McCullagh
Email: hannah.mccullagh@portlandpr.co.uk
Direct: +44 (0)20 7842 0147
Main: +44 (0)20 7842 0123
Mobile: +44 (0)7739 147 841

For more information about the Mo Ibrahim Foundation or the Ibrahim Prize, or to request specific resources for coverage please contact:
Risha Chande
Email: chande.r@moibrahimfoundation.org
Direct: +44 (0)20 7535 5063
Mobile: +44 (0)7817 723 720

Ziara ya Rais Karume nchini China


Rais wa Zanzi bar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,akiwa na mazungmzo na Naibu Meya wa jiji la Shangai China, Tang Deng Jie jana



Rais wa Zanzi bar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,akisalimiana na Naibu Meya wa Mjini Shangai China Tang Deng Jie,akiwa Ziarani Nchini China,(katikati) Ni Mke wa Rais Mama Shadya Karume.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akisalimiana na Balozi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Watu wa China Zhang Hong Xi, katika Uwanja wa Ndege Shanghai, katika ziara yake ya kiserikali , amefuatana na Mkewe Mama Shadya Karume,pamoja na Maofisa wengine wa Serikali,katika mapokezi hayo alikuwepo. Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Ramadhan Mapuri.
Picha na Abadalah Haji China.


Rais wa Zanzi bar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Amani Abeid Karume,na Mkewe Mama Shadya Karume wakiangalia maonesho katika moja ya mabada ya monesho ya Expo 2010,Mjini Shangai akiwa ziarani Nchini humo.

Saturday, May 22, 2010

Pay Trade Service launched in Tanzania


Tanzania Investment Centre (TIC) Board Chairman, Ambassador Elly Mtango (right) shaking hand with President and Executive Officer of the Carview Corporation of Japan, Motoi "Murimi" Matsumoto during the launch of a Pay Trade Service a Carview's argent firm in Tanzania at the occasion at New Africa Hotel in Dar es salaam today.

Trade Carview Japan today officially launched their Pay Trade Service in Tanzania to safeguard the interests of motor vehicle buyers who make advance payments to importers and to legitimize such transactions.

Trade Carview Director, Mr Motoi Matsumoto, and Deputy Director Mr Nobuaki Chatani, presided over the launch and gave their assurances to motor vehicle importers and members of the Media that the service would boost the car importation business.

Mr Matsumoto announced that Trade Carview will also open offices in Kenya, Tanzania and Uganda from where they will extend their Pay Trade Service to the rest of East Africa where car buyers will no longer lose money through the advance payments system.


Why Use Pay Trade
Most of the sellers on Trade carview request buyers to pay 100% upfront before shipment, but buyers often feel unsecure to transfer such big amount without any guarantee. Transferring your funds through Pay Trade is like purchasing insurance for the item you ordered.

When you make payments through Pay Trade, your money is held by Trade carview in a secure manner and the money is only released to the seller after Trade carview confirms the shipment is complete.

Dispute Resolution
If the item that was not shipped or what you ordered (not the same chassis No./VIN number) or if the seller failed to ship the car within 60 days from the date of confirmation of the payment, Trade carview will take over the matter immediately. The buyer can also submit a Refund Request and Trade carview will contact both parties and mediate on the basis of evidence provided.
All decisions made by Trade carview are final.

The launch of this service is an added advantage to buyers because they will now be able to track their payments and delivery of their orders.

OBAMA KUTUA BONGO KESHO NA KUPIGASHOO MSASANI CLUB


Presidaa wa Vijana masauti Christian Bella anategemewa kutua Nchini Jumapili ya Kesho kwa ndege ya shirika la Ndege la kenya.

Katika msafara huo Bella ataambatana na wacheza show wanne wapya wa Akudo impact na moja kwa moja wataelekea katika ukumbi wa Msasani Beach Club kawe kuungana na wanamuziki wengine wa Akudo ili kuendeleza burudani katika bonanza lao la kimataifa

akizungumzia hilo kwa njia ya Simu bella amesema wacheza show hao walikuwa kambini takribani kwa wiki tatu na sasa wanazijua stail zote za Akudo na kesho nitawatambulisha kwenye bonanza letu na watacheza stail zote za vijana wa Masauti , pia nime wamiss wapenzi wangu hivyo wategemee makubwa kutoka kwangu siku ya kesho.

JAKAYA ALIPOPOKEA FARU KUTOKA AFRIKA KUSINI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia SANAMU ya Faru wakati wa sherehe za kuwapokea Faru Watano kati ya 32 kutoka Afrika ya Kusini.Sherehe za kuwapokea Faru hao walioko katika Kontena katika gari nyuma ya Rais zilifanyika katika uwaanja wa ndege wa Seronera katika mbuga ya wanyama Serengeti jana jioni .
Kulia ni Waziri wa mazignira wa Afrika ya kusini Buyelwa Sonjica aliyekabidhi Faru hao kwa niaba ya Serkali ya Afrika ya Kusini.Kushoto ni Waziri wa Utalii na maliasili Shamsa Mwangunga(Picha na Freddy maro)

ONYESHO MAALUM LA FILAMU YA LOVELY GAMBLE


ONYESHO MAALUM LA FILAMU £OVELY GAMBLE TAREHE 29TH OF MAY 2010. KARIBUNI KUCHANGIA YATIMA WALIOATHIRIKA NA UKIMWI TANZANIA NA JUMUIA YETU YA TANZANIA.
WATOTO HAWA WANAANGALIWA NA TANZANIA MITINDO HOUSE INAYOENDESHA SHUGHULI ZAKE TANZANIA.
JUMAMOSI TAREHE 29/05/2010.
SAA 12 Jioni MPAKA SAA 5NA NUSU Usiku.
WYCLIFFE VENUE,
233 KINGS ROAD,
READING, RG1 4LS.
VILEVILE KUTAKUWA NA CHAKULA, VINYWAJI, BURUDANI YA MIZIKI NA VICHEKESHO . NYOTE MNAKARIBISHWA NA KUFIKA KWENU NDIO KUFANIKISHA SHUGHULI HII. TUNAWAOMBA MJE KUSAIDIA WATOTO HAWA NA JUMUIYA YETUWETU.
DRESS CODE: LADIES: DRESS SEXY & GENTS: SMART
MUSIC: LIVE MUSIC, AFRO BEAT, BONGO FLAVOR, HIP HOP, MDUARA AND RNB
TIKETI ZIPO KUANZIA £10 KWA VITI VYA VIP’s NA £5 KWA VITI VYA KAWAIDA.
TIKETI ZINAPATIKANA –
SWIFT FREIGHTS UK (TZUK) – LONDON 0208 801 9800
AFRICANS IN LONDON TV (TINA) – LONDON
MOUDY – LONDON 078884441222
KAYE MARIE – LEICESTER 0794665430
BARAKA - LEICESTER 07909260435
BONGO FLAVOUR – READING 0118 958 5878
VINCENT BAR – READING 0118 959 3130
TANZANIA ASSOCIATION – READING 07865673756
FRANK – READING 07865594576
INFO:urbanpulsecreative@googlemail.com www.wix.com/effeort111/urbanpulse-tmh http://www.youtube.com/watch?v=zNltrl096hU .

MAMA KIKWETE CHINA LEO

e
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA,Mama Salma Kikwete akimkabidhi zawadi ya kinyago cha ujamaa Mheshimiwa Wang Zhizheng, 'Vice-chairperson, Chinese People's Political Consultative Committee'aliyemwandalia Mama Salma Kikwete chakula cha mchana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye mjadala wa "Leading Government's Reach to women" pamoja na Mheshimiwa Nguyen Thi Doan,Makamu wa Rais wa Vietnam,katikati, na mwishoni ni Moderator Yang Lan, Afisa Mtendaji Mkuu na Mmiliki wa 'Sun Media Group'nchini China .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kwenye ufunguzi rasmi wa mkutano wa 20 wa "Global Summit of Women" kwenye ukumbi wa 'Great hall of people'huko Beijing nchini China tarehe 20.5.2010. Aliyekaa kushoto kwa Mama Salma ni Mheshimiwa Maud Olofsson, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Sweden.

Na Mwandishi Maalum,Beijing

MKE wa Rais Mama Salma Kikwete leo atahutubia mkutano wa wanawake wa dunia katika kuelezea mafanikio aliyoyapata katika taasisi yake ya wanawake na maendeleo (WAMA) na juhudi zake binafsi za kusaidia ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.

Mama Kikwete ambae ametajwa kuwa mfano bora kwa wake wa marais wa Afrika kufuatia taasisi yake ya WAMA kujikita zaidi katika kusaidia jamii na hasa jitihada zake binafsi za kusaidia wanawake,afya, na watoto wanaoishio katika mazingira hatarishi.

Katika mkutano huu wa dunia unafikia kilele chake leo, katika ukumbi wa Marriot city Hall uliopo katikati ya jiji la Beijing na karibu wajumbe 1000 wanaohudhulia mkutano huo wana hamu kubwa ya kusikia mafanikio aliyopata Mama Kikwete katika kutimiza malengo yake ya WAMA.

Juzi katrika ufunguzi wa mkutano huo, Rais wa Global Summit of Woman, Bibi Irene Natividad alimtaja Mama Kikwete kuwa ni mfano bora wa wake wa marais kutoka Afrika na kusema kuwa jitihada zake binafsi zinaweza kuwa fundisha kwa wake wengine wa marais kutoka Afrika na wanwake wengine wanaopenda kusaidia jamii.

Awali jana mchana Mama Kikwete alialikwa katika mkutano wa kuwatambulisha watu mashuhuri waliohudhulia mkutano huo, lakini asilimia kubwa ya maswali yalielekezwa kwa Mama Kikwete baada ya kutakiwa kueleza kwa nini alinzisha taasisi ya WAMA na madhumuni yake makubwa yalikuwa ni nini.

Akijibu maswali kwa kujiamini , Mama Kikwete Kiwete alisema madhumuni makubwa ya kuanzishwa kwa WAMA ni kumuendeleza mwanamke kielimu, kiafya na kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na wale wanaishi katika mazingira hatarishi.

Alisema kuwa vitu vingi amekuwa akifanya kupitia taasisi yake ya WAMA kusaidia wanawake wa Kitanzania ikiwemo suala la elimu kwa kuwa ndiyo njia pekee ambayo inaweza kumkwamua mwanamke katika maisha ya chini na hili amekuwa ameanza kwa wasichana wadogo kuwasisitiza umuhimu wa elimu na kujiepusha na mimba za utotoni na hususan swala la kujiepusha na ugongwa wa ukimwi.

Pia alisema katika serikali ya awamnu ya nne inayoongwa na mumewe imeweza kupiga hatua kubwa katika suala la kumtetea mwanamke, kwani wanawake wengi wamekuwa wakipewa nafasi za uongozi kwa asilimia kubwa na hata masuala mbalimbali ya kimaendeleo.

Mama Kikwete aliendelea kusema kuwa mbali ya hiyo serikali imeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa benki ya maendeleo ya wanawake ambayo itakuwa hatua muafaka ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

“Ni ushahidi mwingine kwamba serikali yetu inawajali wanawake wa Tanzania na inayodhaamira ya dhati ya kuinua hali zao za kimaisha na kuwepo kwa benkihiyo kumetoa fursa kwa wanawake wa Tanzania kutumia huduma zake za kujiletea maendeleo na kuondokana na umaskini.

Awali mchana jana alikutana na viongozi wa chama cha wafanyabishara wanawake wa China na wale wa Tanzania katika kubadilishana mawazo na kuona uwezekano wa kusiadia katika masuala mbalimbali ya kibiashara katika ya nchi hizi mbili.

Friday, May 21, 2010

WAPIGA PICHA WAKIFANYA UTUNDU !!!



Wapiga picha kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakichukua picha za matukio kwenye tamasha la nyimbo za injili ambalo lilifanyika Desemba 25 mwaka jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jublee . Tamasha hilo la aina yake liliandaliwa na kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam.
Hawa ni baadhi ya watu ambao walihudhulia tamasha hilo ambalo lilifana kweli kweli.

RAIS KIKWETE AMEMTEUA BWANA DEOS MNDEME KUWA POSTA MASTA MKUU WA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Deos Mndeme kuwa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania kuanzia mwezi Aprili, 2010.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dkt Florens Turuka imesema kuwa, Bwana Mndeme alikuwa kaimu Posta Masta mkuu kwa kipindi kisichopungua miaka miwili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kabla ya uteuzi huo Bwana Mndeme alikuwa ni mfanyakazi wa shirika hilo kwa muda wa takribani miaka thelathini lililoanzishwa kufuatia kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Simu la Afrika Mashariki.

USIKU WA REGGAE IRINGA MJINI WIKI HII




.

Habari zenu.
Mnakaribishwa kwenye USIKU WA REGGAE. Burudani ya muziki wa LIVE hapa Iringa mjini kwenye ukumbi wa Idydc..Jumapili hii saa 2 usiku hadi usiku wa manane.
WOTE mnakaribishwa.

fainali Zain Africa Challenge 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

May 20, 2010

Kenya yaingiza vyuo vitatu nusu fainali Zain Africa Challenge

Vyuo vitatu kutoka nchini Kenya vimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mashindano yanayoendelea ya Zain Africa Challenge, chemsha bongo ya mtoano ya kimataifa ya Vyuo vikuu kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika.

Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Africa Nazarene, Chuo kikuu cha Egerton na Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta. Chuo Kikuu cha Makerere ndiyo chuo pekee kutoka nje ya Kenya ambaco kimefuzu hatua ya nusu fainali pia.

Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, Chuo kikuu cha Makerere kutoka Uganda kitakutana na Chuo Kikuu cha Africa Nazarene cha Kenya katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali utakaofanyika jumapili ya wiki hii.

Mchuano mwingine wa nusu fanali utawakutanisha Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta na Chuo Kikuu cha Egerton vyote kutoka Kenya.

Vyuo Vikuu hivyo vinne vilivyofuzu kuingia katika hatua ya nusu fainali fainali za ZAC ndivyo vinavyowania nafasi ya kuingia fainali ambapo mshindi atapata kitita cha dola za marekani 50,000.

Watazamaji wa Zain Afrika Challenge bado wanafursa ya kushiriki katika mchezo wa Zain kupitia SMS kwa kujibu maswali yanayoulizwa wakati wa mtoano na kujishindia zawadi ya simu mpya za mkononi aina ya Nokia N97 yenye thamani ya zaidi ya shilingi laki nane.

Ili kushiriki katika mchezo wa ZAC watu wenye simu za mkononi watatuma majibu ya swali litakaloulizwa kwenda namba 15315.

Jumla ya Vyuo Vikuu 100 kutoka nchi nane barani Africa ambazo ni Ghana, Kenya, Malawi, Nigeria, Tanzania, Uganda na Zambia vilichuana katika mtoano wa kitaifa kabla ya kuingia raundi ya kwanza ya fainali ya mtoano wa ZAC nchini Uganda.

Programu ya Zain Afrika Challenge ni sehemu ya juhudi za Zain zinazolenga kuboresha sekta ya elimu na inadhihirisha dhamira ya Zain ya kuleta Ulimwengu Maridhawa kwa wateja wa Zain.

Thursday, May 20, 2010

Presidnt Kikwete meets the EU Foreign Minister Baroness Ashton and chairs CCM NEC meeting


President Jakaya Mrisho Kikwete chairing the Central Committee CC of The Chama Cha Mapinduzi in Dar es Salaam today morning.Others in the picture are Zanzibar's President Amani Abeid Karume,Vice President Dr. Ali Mohamed Shein and The SMZ Cheif Minister Shamsi Vuai Nahodha.On the Left is CCM Secretary General Yusuf Makamba (photos by Freddy Maro).

Align Center


President Jakaya Mrisho Kikwete in conversation with EU Foreign Minister Baroness Cathy Ashton at Dar es Salaam State House in Dar es Salaam today morning.

MSAKO DHIDI YA WAHUJUMU KAZI ZA WASANII


KURASA YA MICHEZO WIKI HII


UKURASA WA KWANZA WA DIRA WIKI HII


African Reggae meets Northern Blues East Africa Tour


Kasheshe la kutaka kulipuliwa ubalozi wa marekani jumapili



Tamko kwa Vyombo vya Habari
Mei 20, 2010

Siku ya Jumapili, tarehe 16 Mei, mnamo saa 2.30 usiku, mvulana mwenye umri wa miaka 15 alikimbia na kumpita mlinzi aliyekuwa mbele ya Ubalozi wa Marekani, akawasha moto kwenye chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na kisha kuirusha chini ya moja ya malori mawili ya kubebea maji yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ukuta wa Ubalozi.
Chupa hiyo ilivunjika lakini haikuweza kulipua moto. Walinzi wa Kampuni ya KK wanaolinda ubalozini hapo walimkamata mara moja kijana huyo kabla hajaweza kurusha chupa ya pili. Hakukuwa na mtu yeyote aliyejeruhiwa wala mali yoyote iliyoharibiwa katika tukio hilo. Askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania aliwasili sehemu ya tukio sekunde chache baadaye na kumkamata mtuhumiwa. Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi.

Baadhi ya maelezo yanayotolewa kuhusu tukio hili si sahihi, yamekuzwa na kutiwa chumvi mno na yasiyo ya kweli, yakidai kuwa mvulana huyo aliingia ndani ya ubalozi. Hii si kweli. Hakukuwa na mtu yeyote aliyeweza kuingia ndani ya Ubalozi wa Marekani.
Taratibu zetu za kiusalama za kuzuia wahalifu kuingia ubalozini zilidhihirisha ufanisi wake hapo Mei 16. Walinzi wa kampuni ya KK na Polisi wa Tanzania walishughulikia suala hili kwa weledi mkubwa.
Tunawashukuru sana.

SWAGGA NITE SWAGGA NITE SUN30Th MAY BANK HOLIDAY WKEND AT FACE CLUB READING





wakuuu naomba tuwakumbushe ime baki week moja


BONGODEEJAYS in collaboration with INFINITY ENTS proudly Presents SWAGGA NITE IN READING ONE NITE ONLY NEVER LIKE BEFORE


WE BACK THIS TIME EVEN BIGGER....SUN 30ThMAY2010 BANK HOLIDAY WEEK END.

Last time we brought ALI KIBA & T.I.D ... and he absolutely smashed the night.For some of you that remember...it was a memorable event and a Big Success..So now we goin Hard..OH YEH..!..

THIS TIME SWAGGA NITE SWAGGA NITE!!! LOTS OF INTERTAINMENT & PRIZES TO BE WON INCL BOTTLE OF CHAMPAGNE FOR THE BEST COUPLES OF THE NITE .

DOOR OPEN 10PM TILL 5AME
ENTRY £ 7 BEFORE 12 MIDNIGHT £10 AFTER

So make sure your there and tel a friend to tel a friend.. SUN 30ThMAY2010 ...
BANK HOLIDAY FACE NITE CLUB....
NO WORK ' NO UNI..........
PAY DAY.......................SO NO EXCUSES' WATSOEVA!

4 MORE DETAILS CONT 07853482158 OR 07576729964

**************www.bongodeejays.blogspot.com***************

Wednesday, May 19, 2010

Tamasha la Kimataifa la Injili la Desemba 25






KAMPUNI ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, iliaandaa tamasha la kimataifa la nyimbo za injili, lililofanyika Desemba 25, mwaka jana kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Mimi Alex Msama ndiye nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, wa tamasha hilo la aina yake ambapo tamasha hilo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwaunganisha waimbaji kutoka nchi za Kenya, Malawi, Uganda, Burundi Zambia na Afrika Kusini.

Lengo la tamasha hilo ilikuwa kuwasaidia watu wenye ulemavu na yatima na wengine wenye mahitaji ambao wanapaswa kusaidiwa katika jamii.

Ujue kuna baadhi ya watu wenye ulemavu ambao wanahitaji misaada mbalimbali, kwa mfano baiskeli, hivyo kampuni yangu ililiona hilo, hivyo tukapanga kuelekeza nguvu kwa walemavu wa mikoani .

Fikiria kuna wengine wanatamani kusoma, lakini kwa kukosa usafiri na huduma nyingine muhimu, wanashindwa, hivyo tumeona ni vizuri kama tutawakumbuka.

Binafsi nimechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa huu wa injili nikiwa kama muasisi wa matamasha ya injili hapa Tanzania , katika tamasha hilo, pia kulikuwa na waimbaji wapya walioingia katika albamu ya Haleluya Collections Volume 5, wakiwamo kutoka Tanzania.

Kamati imeamua kufanya matamasha mara mbili kwa mwaka ikiwa ni kufanyia kazi maoni ya wapenzi na mashabiki wa muziki huo. Kuhusu misaada kwa makundi mbalimbali ya kijamii, kamati yangu imekuwa ikifanya hivyo ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kusaidia wenye mahitaji katika jamii.

Alisema, kamati hiyo imekuwa ikimuomba Mungu azidi kuijalia uwezo kwani lengo ni kugawa baiskeli 100 kila mwaka badala ya 70, ilizowahi kugawa na kusomesha yatima. Mbali ya baiskeli, kamati hiyo imewahi kutoa vitanda vya wagonjwa katika hospitali mbalimbali nchini ingawa kwa kipindi hicho hatukuwa tukitangaza hadi pale tuliposhauriwa kufanya hivyo.

Hivyo, kuanzia mwaka jana tumeanza kutangaza hata mapato katika matamasha mbalimbali ili kuwa wazi zaidi, tunadhani kuwa itatujengea imani zaidi kwa jamii.

Aidha, natumia fursa hii kutoa wito kwa watu mbalimbali katika jamii kuguswa na suala hilo, kwani linalenga kusaidia makundi maalumu katika jamii. Sambamba na hilo, natoa wito pia kwa jamii kuunga mkono juhudi za kamati hiyo kwa kununua albamu ya Haleluya Volume 5 iliyoko madukani kwa wakati .

BWANA AWE NANYI.

Monday, May 17, 2010

NI ROSE MHANDO HUYU JUKWAANI TAMASHA LA HALELUYA








Rose Mhando hapa alikuwa anaimba kwa hisia na unaweza kuona jinsi nyimbo za kiroho zinavyo muweka kwenye hali ya namna hii .
Ukumbi ni Diamond na ilikuwa Tamasha la Haleluya ambapo yeye ni mmojawapo wa wasanii walibahatika kuimba na nyimbo kuvuta hisia za watazamaji , ni muimba mzoefu na aliyepita kwenye changamoto nyingi kufika hapa alipo.

KILA MTU ANAFURAHI UKUMBINI







Kazi ilikuwa kubwa na karibu kila mtu ndani ya ukumbi alikuwa amefurahi huku nyimbo za kumsifu mungu zikitawala.Furaha ilikuwa kubwa katika kila nafsi ya mtu, hapa unaona jinsi hali jinsi hali ya kila mmoja ilivyokuwa siku hiyo ndani ya ukumbi huu.

MTOTO KACHANGAMKA!!!




Huyu mtoto siku hiyo yaani Desemba 25 mwaka jana alichangamka mno hadi watu wote ndani ya ukumbi wakafurahi.Jamani si mnamuona wenyewe?!

NI MIMI NA SPIKA MH.SAMWEL SITTA DIAMOND JUBLEE


Nakumbuka ilikuwa tarehe 25 Desemba mwaka jana ndani ya ukumbi wa Diamond Jublee ambapo kampuni yangu Msama Promotion iliandaa tamasha kubwa la nyimbo za injili .Mh Spika Samwel Sitta ndiye alikuwa mgeni rasmi na shughuli ilifanyika vema mno.

KARIBUNI!!!

KARIBUNI !!!
Naitwa Alex Mwita Msama ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion yeye ofisi maeneo ya Block41, Kinondoni,jijini Dar es Salaam.Nimeamua kuanzisha blugu hii ili watu na jamii nzima kwa ujula muweze kupata kwa urahisi habari zinazonihusu mimi binafsi na taarifa za matamasha na masuala mengine mengi yanayonihusu.Hivyo, karibuni tujumuike na naahidi kuwa bize sana hapa!!!